SIRI YA KIKWETE YA VUJA

Mwenyekiti wa CCM, Jakaya Kikwete
VIGOGO watatu wa Chama cha Mapinduzi, akiwamo waziri mmoja, wanaotajwa kuweza kuwania kuteuliwa na chama hicho kugombea urais mwaka 2015, wanatajwa kuhusika kugawa fedha kwa baadhi ya wenyeviti na makatibu wa wilaya wa CCM, waliokutanishwa mjini Dodoma wiki iliyopita, Raia Mwema, limeelezwa.

Kwa mujibu wa vyanzo vyetu vya uhakika vya habari, wagombea watatu watarajiwa wa urais wanahusika. Katika orodha hiyo ya wagombea hao watatu, anayeongoza ni yule aliyekuwa akitoa Sh 400,000 kwa baadhi ya makatibu wa wilaya waliohudhuria semina ya mafunzo iliyofanyika mjini Dodoma wiki iliyopita.

Mgombea huyo amewahi kuwa na wadhifa mkubwa kitaifa ambaye ni kutoka kanda ya kaskazini (jina linahifadhiwa kwa sasa). Wengine ni pamoja na Waziri wa sasa katika Serikali ya Kikwete, ambaye anatokea Kanda ya Ziwa.

Mbali na hao, mwingine anayehusika ni aliyepata kuwa Waziri kijana kutoka Kanda ya Ziwa.

Kwa upande wa mgombea kutoka Kanda ya Kaskazini, timu yake ya kugawa fedha ilikuwa ikigawa fedha hizo kupitia kwa baadhi ya makatibu wa wilaya wa CCM.

“Ilikuwa anaitwa katibu wa wilaya ama anapewa fedha taslimu shilingi 400,000 au anatumiwa katika simu yake ya mkononi. Kati ya hizo shilingi 400,000, anatakiwa kutoa shilingi 200,000 na kumpa mwenyekiti wake wa chama wa wilaya. Wanasema ni fedha tu za kuwasaidia ‘maisha’ hapo Dodoma lakini nyuma yake ni mpango wa kusaka wapiga kura wa mkutano mkuu 2015,” kinaeleza chanzo chetu cha uhakika cha habari.

Kwa mujibu wa utaratibu wa CCM, kila wilaya inatoa wajumbe 10 wanaoingia katika mkutano huu wa chama hicho na kila wilaya inaongozwa na mwenyekiti na katibu wa chama.

Safu ya viongozi wajuu wa wilaya za CCM mbali na mwenyekiti na katibu wake, inatajwa pia kumhusisha mbunge.

“Kwa hiyo, utaona kwamba mgombea mwenye malengo akifanikiwa kumshawishi kwa njia yoyote mwenyekiti na katibu wa chama wilaya, pamoja na mbunge anakuwa amejenga mazingira mazuri, kwa sababu hao ndiyo wenye ushawishi mkubwa kwa wajumbe wengine saba kutoka wilaya husika ambao wanaingia kwenye mkutano mkuu,” kinaeleza chanzo chetu kingine cha habari.

Taarifa zaidi zinabainisha kwamba, hakuna kigogo aliyekuwa akitoa fedha chini ya shilingi 100,000 kwa baadhi ya wajumbe hao ambao idadi yao ya jumla ni 445.

Kikwete achukizwa

Ni kutokana na hali hiyo ya kusambaza fedha za rushwa kwa njia ya simu au taslimu, inadaiwa kwamba Rais Jakaya Kikwete hakuweza kuficha hasira zake na badala yake, aliwaeleza wajumbe wa mkutano huo kwamba chama hicho kinaweza kuanguka katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015, iwapo hakitajiepusha na rushwa.

Rais Kikwete ananukuliwa akisema; “Kama hatutabadilika katika suala la rushwa mwaka 2015 tutakuwa na wakati mgumu sana na kama mwaka huo tutafanikiwa kuishika serikali, basi mwaka 2020 hatutarudi tena madarakani.

“Najua rushwa ipo na mnaendelea kupokea shilingi laki mbili za airtime (muda wa mawasiliano), ndugu zangu hatutafika ama wengine watavuka na wengine kukwama,” amesema Mwenyekiti huyo wa CCM.

Katika kuthibitisha ugawaji huo wa rushwa aliendelea kuwaeleza wenyeviti na makatibu hao wa CCM akisema; “Viongozi wa chama ndio mmekuwa mawakala wa kusambaza rushwa bila hata aibu. Nawaombeni tubadilike, kama tutaendelea hivi hali yetu itakuwa ngumu sana katika chaguzi mbalimbali, nawaambieni.”

Beki Tatu na wenzake watibua mpango

Taarifa zinaeleza kwamba kati ya wanachama na viongozi wa CCM waligoma na kutibua mpango huo wa kugawa rushwa ni pamoja na kiongozi kutoka mkoani Mara, maarufu kwa jina la Beki Tatu.

Inaelezwa kwamba huyo, pamoja na baadhi ya wenzake waligoma kununulika na kuchukizwa na viongozi wakuu wanaohusika katika mpango huo.

Changamoto kwa Mangula

Kwa sasa, Makamu Mwenyekiti wa CCM Mzee Philip Mangula amepewa mtihani mwingine wa kujisafisha baada ya mtihani wa awali kuanguka licha ya kutoa ahadi ya miezi sita ya kushughulikia watu walioaminika wameingia madarakani ndani ya CCM kwa rushwa.

Chanzo chetu cha habari kinaeleza kwamba ushahidi wa kutosha umekusanywa na baadhi ya wahusika wa kusambaza rushwa wiki iliyopita mjini Dodoma watachukuliwa hatua kali.

“Mangula ni kama amepewa fursa ya kujisafisha baada ya kukwama kwa ahadi yake ya awali ya kushughulikia waliongia madarakani katika uchaguzi ndani ya chama kwa njia ya rushwa. Sasa hivi amepewa na ushahidi wa wazi, uchaguzi ni wake, kuwashughulikia au kuwaacha na aendelee kuonekana kiongozi asiyeweza kutumia madaraka aliyopewa,” anaeleza mmoja wa viongozi wastaafu ndani ya CCM ambaye hakutaka jina lake liandikwe gazetini.

Maadili na Katiba Mpya

Wagombea hao wa urais watarajiwa ambao huenda wakagombea katika kipindi ambacho nchi imeridhia kutumika kwa Katiba Mpya, inayotarajiwa kuzinduliwa Aprili, mwakani, awamu ya kwanza ya rasimu ya Katiba hiyo mpya imetambua moja kwa moja, maadili ya uongozi na uwajibikaji.

Katika sura ya 13 ya Katiba Mpya, Ibara ya 189 inabainisha majukumu ya jumla ya Tume ya Maadili ya Uongozi na Uwajibikaji kuwa ni kufuatilia na kuchunguza tabia na mwenendo wa viongozi na watumishi wa umma kwa madhumuni ya kusimamia na kuhakikisha kuwa maadili ya uongozi wa umma na miiko ya uongozi wa umma inazingatiwa, inalindwa na kuheshimiwa katika utumishi wa serikali, Bunge, Mahakama, taasisi na idara nyingine zote za umma.

Lakini sehemu ya 2(b) ya Ibara hiyo ya 189 inazidi kuanisha majukumu mahsusi ya Tume kuwa ni kufanya upekuzi na kufuatilia kumbukumbu za wanaoomba nafasi za uongozi wa umma.

Vile vile sehemu ya 2(f) ya Ibara hiyo ya 189 inaeleza kazi mahsusi ya Tume ya Maadili kuwa ni; “kufanya uchambuzi yakinifu kwa viongozi wa umma wanaopewa dhamana kabla ya kuingia madarakani.”

Kwa hiyo, kwa ujumla kama maadili hayo yataendelea kuwamo katika Rasimu ya Katiba Mpya itakayowasilishwa bungeni na endapo rasimu hiyo itaridhiwa na Bunge la Katiba ikiwa na mapendekezo hayo na kisha wananchi kupigia kura ya ndiyo rasimu hiyo ili kuwa Katiba Mpya, basi, vigogo hao wanaotajwa sasa wanaweza kujikuta wakikwamishwa na Tume ya Maadili, ambayo itakuwa huru ikipewa mamlaka ya moja kwa moja na Katiba ya nchi

Kwa hiyo, kwa ujumla kama maadili hayo yataendelea kuwamo katika Rasimu ya Katiba Mpya itakayowasilishwa bungeni na endapo rasimu hiyo itaridhiwa na Bunge la Katiba ikiwa na mapendekezo hayo na kisha wananchi kupigia kura ya ndiyo rasimu hiyo ili kuwa Katiba Mpya, basi, vigogo hao wanaotajwa sasa wanaweza kujikuta wakikwamishwa na Tume ya Maadili, ambayo itakuwa huru ikipewa mamlaka ya moja kwa moja na Katiba ya nchi - 
CHANZO RAIA MWEMA

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright WORLD OF TODAY Published.. Blogger Templates
Back To Top