
Chama
cha Demokrasia na maendeleo CHADEMA Kanda ya Ziwa Mashariki leo
kimewavua nyadhifa zao viongozi wake watano wa jimbo la Kahama kwa
makosa mbalimbali ikiwa ni pamoja na kukiuka taratibu za chama hicho.
Uamuzi
huo umetolewa na Mratibu wa Chedema Kanda ya Ziwa Mashariki Renatus
Nzemo katika kikao kilichofanyika katika ofisi ya Kanda ya Ziwa
Mashariki na kupitia mazimio hayo kabla ya kutoa uamuzi.
Viongozi
waliovuliwa nyadhfa zao ni Mwenyekiti wa jimbo la Kahama Israel
Barikiel, Katibu wa Jimbo Vicent Kilukilwa, Katibu Mwenezi wa jimbo
Bobson Wambura, Mwenyekiti Bawacha Kasigwa Adram na Mwenyekiti Bavicha
Benedict Shija.
Katika Barua yake aliyoiandika kwa viongozi hao, Nzemo amesema viongozi
hao wanakabiliwa na tuhuma za kikiuka tamko la kamati kuu ya chama
lililowazuaia wanachama wote kushirikiana na aliyekuwa naibu katika mkuu
wa chama hiccho Zitto Kabwe.
Tuhuma
zingine ni kushiriki kampeni za uchaguzi mdogo katika kata ya Ubagwe
kupitia chama cha TADEA, huku viongozi hao wakipita na kujinadi kuwa
wako tayari kumfuata Zitto popote atakapokuwa.
Aidha
Nzemo amesema viongozi hao wamekuwa wakitumia nembo ya CHADEMA kunadi
chama kingine cha Alliance for change and Transparency (ACT), kinyume
cha maadili ya CHADEMA katika katiba yake ya mwaka 2006.
Nzemo
amesema kutokana na tuhuma hizo na zile zilizotolewa na baraza la
mashauriano wilaya ya Kahama, viongozi hao wanatakiwa kukabidha ofisi na
vifaa vya chama kwa baraza la wazee jimbo la Kahama mara wapatapo barua
hizo.Chanzo.........
No comments:
Post a Comment