MAAJABU YA GHOROFA NNE JIJINI DAR.Zinatumia umeme zaidi ya Mkoa wa Mtwara

 





Dar es Salaam. Ghorofa nne za kisasa zilizopo Dar es Salaam, zinatumia kiasi kikubwa cha umeme kuliko ule unaotumiwa katika Mkoa wa Mtwara.


Majengo manne ya PSPF Twin Tower, Uhuru Height, Viva Tower na Benjamin Mkapa Tower yote kwa pamoja yanatumia megawati 12 za umeme wakati mkoa huo unatumia megawati nane.


Kiasi hicho cha umeme kinachotumiwa na majengo hayo ni karibu sawa na umeme unaotumiwa na mkoa huo na Lindi kwa pamoja.


Aidha, majengo matatu ya PSPF Twin Tower, Uhuru Height na Viva Tower kwa pamoja yanatumia umeme mwingi kuliko ule unaotumiwa na baadhi ya mikoa nchini kama Ruvuma, Manyara, Singida, Kigoma na Rukwa.


Akizungumza katika mahojiano maalumu hivi karibuni, Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania Tanesco, Felchesmi Mramba alisema PSPF peke yake linahitaji megawati tano na Uhuru Height megawati 2.5, Viva Tower megawati 2.5 na Benjamin Mkapa Tower megawati mbili.


Alitaja matumizi ya umeme katika mikoa hiyo na megawati zake kwenye mabano kuwa ni Manyara (10) Mtwara (8), Singida (7), Lindi (5.5), Kigoma (6), Ruvuma (4.7) na Rukwa (6.8).


Alisema Dar es Salaam inaongoza kwa kutumia umeme mwingi na kwamba mahitaji ya nishati hiyo yamekuwa yakiongezeka kutokana na ukuaji wa haraka wa sekta ya ujenzi.


Dar es Salaam pekee, kwa mujibu wa takwimu za Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) matumizi yake ni kati ya megawati 450 na 500 kwa siku, kiasi ambacho ni zaidi ya nusu ya umeme unaozalishwa na shirika hilo.


Alisema hivi sasa umeme unaozalishwa ni wastani wa megawati 1,100, huku sehemu kubwa ya nishati hiyo ikitokana na mitambo inayotumia gesi na mafuta.


Kutokana na hali hiyo, alisema Tanesco imeamua kutekeleza miradi 13 ya ujenzi na ukarabati wa miundombinu ya umeme ikiwamo kuongeza uwezo wa njia za kusambaza na kukarabati. Pia kujenga vituo vipya vya kupozea umeme katika sehemu mbalimbali za Dar es Salaam.


“Baadhi ya majengo makubwa Dar es Salaam yanahitaji umeme mwingi. Unakuta jengo moja kama haya maghorofa linahitaji megawati nyingi za umeme kuliko zinazotumiwa na baadhi ya mikoa,” alisema Mramba na kuongeza:


“Ndiyo maana tunatekeleza miradi mingi ya kuongeza uwezo wa njia za kusambaza umeme maana mfumo tulionao sasa ni chakavu na hauwezi kuhimili kiasi cha umeme kinachotakiwa na watumiaji wa makundi mbalimbali.” soma zaidi..............

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright WORLD OF TODAY Published.. Blogger Templates
Back To Top