
1. Edward Mwanja, mfamasia mstaafu.
Umewaagiza wananchi wasichangie miradi yao ya maendeleo kwa madai Serikali ina fedha za kutosha za kugharamia, mbona hadi sasa hujahimiza Serikali ilete hizo fedha pamoja na za ujenzi wa maabara?
Jibu: Kwa taarifa yako katika jimbo letu kila shule ya kata inajengwa na pia maabara zinajengwa kwa fedha za Serikali. Hivi sasa kuna zilizoko katika ngazi ya lenta nyingine kwenye msingi na yote hiyo ni fedha ya Serikali. Sisi tumesema tumechoka kulaghaiwa kwa kuwa Serikali inapaswa kutekeleza majukumu yake. Kila tunapokaa kwenye kikao katika Halmashauri ya Ikungi tunapitisha bajeti ya masuala hayo hivyo hizi za kuchangisha hazipo kwenye bajeti hiyo.
2. Joseph Sungita
Mbona hujatekeleza ahadi yako ya kuhamia na kuishi jimboni kwako?
Jibu: Sijawahi kutoa ahadi ya aina hiyo. Nimewahi kusema nitakuwa nafanya mikutano kila mara. Unayeuliza siyo wa jimboni kwangu kwa sababu jimboni ni nyumbani kwetu. Nina makazi Singida, Dodoma na Dar es Salaam kutokana na kazi ninayofanya.
3. Hugo John
Hadi sasa umefanya mambo gani katika kuinua sekta ya elimu tangu uwe mbunge?
Jibu: Lazima tujue majukumu ya mbunge ni yapi na ya Serikali ni yapi. Mimi mbunge siyo mwenye fedha, Serikali ndiyo yenye fedha ambazo zinapelekwa halmashauri kwa ajili ya shughuli hizo. Kama mbunge na mwenyekiti wa kamati ya mfuko wa maendeleo ya jimbo ambao fedha zake ni kidogo tumeweza kutoa kidogo kwenye elimu kwa kukarabati nyumba za walimu na pia katika miundombinu ya maji.
4. Basil Ntandu read more..........
No comments:
Post a Comment