Nina mke niliyeoa miaka 10 iliyopita. Nimezaa naye watoto 3. Hajawahi kunifanyia kosa lolote. Sijawahi kumkamata na mchepuko japo yeye amenibamba kama mara 2 na michepuko kwenye simu. Lakini kwa zaidi ya miaka miwili sasa, sina raha ya kuendelea kuishi na mke wangu. Kuna roho inaniagiza niachane naye,nioe mke mwingine. Hata huduma ya kitandani sina hamu kabisa.
Nafanya kama mara 1 kwa mwezi napo kwa kujilazimisha tu, wakati mwingine hata miezi mitatu bilabila. Ameshazoea hivyo. Akiwa MP nafurahi sana kwamba napata kisingizio. Siyo kwamba nina mchepuko ninayemalizia haja, hapana! Sina appetite na mke wanguhuyo.
Nikiwa kitandani napenda kumpa mgongo, siyo kumkumbatia. Nina umia sana, sasa naelekea kukubaliana na roho hiyo, nipo naangalia namna ya kulea watoto nikiwa sipo na mke wangu huyo.
Natafuta mbinu za kumwacha. Nimeshawaandaa kisaikolojia nduguzangu ili nikimwacha wasinilaumu. Lakini ukiniuliza amenikosea nini, sina jibu labda nimsingizie! Sijui nimelogwa mie? Sijui imekuwaje.
Naomba ushauri wenu tafadhali.......
TUPE MAONI YAKO HAPA CHINI
No comments:
Post a Comment