WAKATI
Serikali ya Umoja wa Kitaifa (SUK) ikitimiza miaka mitatu, Chama cha
Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimesema mfumo wa serikali hiyo
Zanzibar umeshindwa kudhibiti ufisadi na kuua dhana ya demokrasia ya
vyama vingi.
Hayo
yalisemwa jana na Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA Zanzibar, Hamad Mussa
Yussuf, alipohutubia mkutano wa kampeni za uchagzu mdogo wa Kiembesamaki
zilizofanyika uwanja wa Kiembesamaki na kumnadi mgombea wa chama hicho,
Hasim Juma Issa.
Hamad
alisema tangu kupatikana kwa SUK, dhima ya upinzani imepotea na
kukithiri kwa vitendo vya ubadhirifu na ufisadi, huku Baraza la
Wawakilishi likishindwa kuisimamia serikali katika utekelezaji wa ripoti
za uchunguzi zinazoikaba serikali.
“Baraza la
Wawakilishi Zanzibar limekosa meno, halifanyi kazi kama Bunge la
Muungano ili kuisimamia SMZ, kinahitajika chama mbadala kuingia kwenye
Baraza la Wawakilishi haraka kabla mambo hayajaenda mrama,” alisema
Hamad.
Alizitaja
ripoti za ubadhirifu wa fedha za umma katika Shirika la Umeme Zanzibar
(Zeco), Baraza la Manispaa ya Mji wa Zanzibar (ZMC) mbali na ripoti za
uchunguzi wa uuzaji wa majengo ya serikali yaliouzwa kwa bei ya kutupwa
kinyume cha sheria.
Naibu katibu
mkuu huyo alisema vyama vya CCM na CUF vimepoteza imani kwa wananchi na
sasa ni wakati sahihi kwa Zanzibar kupatikana chama kingine
kitakachopigania masilahi ya wananchi na kuibana serikali.
Vyama vya
CCM na CUF kwa mujibu wa Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984 ndivyo
vinavyounda serikali ya umoja wa kitaifa Zanzibar kutokana na kupata
viti vya uwakilishi na kura za urais kwa asilimia 10.
Kwa upande
wake mgombea wa uwakilishi Hasim Juma Issa, alisema iwapo atachaguliwa
atajenga hospitali itakayohudumia wananchi, usambazaji wa maji safi na
salama na kujenga barabara kwa kiwango cha lami.
Alisema
wabunge na wawakilishi wa CUF wameshindwa kutumia ruzuku ya maendeleo ya
jimbo na idadi kubwa ya wawakilishi na wabunge wamelazimika kufanya
kazi kwenye mikoba kwa kushindwa kujenga ofisi huku wakilipwa sh milioni
25 na sh milioni 10 wanazolipwa wawakilishi.
Post a Comment