DENI LA TAIFA LAONGEZEKA TENA.SOMA HAPA UJUE LIMEFIKA DOLLA NGAPI

HIVI karibuni Waziri wa Fedha na Uchumi Saada Mkuya alisema kuwa Tanzania inakopesheka, kwamba Serikali itaendelea kukopa kwa sababu bado ina sifa za kukopa.

Waziri akasema kuwa deni la taifa limeongezeka na kufikia dola za Marekani bilioni 17.10 (Sh. trilioni 27.04) hadi Desemba mwaka jana.

“ Tunaendelea kukopa na deni linaongezeka. Linaongezeka kwa mikopo inayochukuliwa na ile ambayo haijalipwa. Linaongezeka kwa kuwa nchi bado inaendelea kukopa,” alisema Mkuya.

Halafu akadokeza kuwa hivi sasa Tanzania imejikita zaidi katika kukopa mikopo yenye masharti ya kibiashara ambayo ni tofauti na mikopo yenye masharti nafuu. Yaani tunakopa kutoka benki za kibiashara zenye riba zaidi.

Anachosema Mkuya ni kuwa tunashindwa kutekeleza Bajeti ya Serikali na kisha tunaishia kukopa. Kwa mfano, katika Bajeti ya mwaka 2013, mapato ya ndani yalikuwa Sh. 4.8 trilioni wakati tulipanga kukusanya Sh 5.7 trilioni. Kwa nini? Hili halikuzungumzwa na Mkuya.

Hata mwaka 2009/10 wakati wa waziri Mustafa Mkullo ilitangazwa kuwa katika robo ya kwanza TRA ilishindwa kukusanya shilingi 100 bilioni zilizokusudiwa katika bajeti. Mkullo akatuambia tusitaharuki.

Watanzania wanapaswa wataharuki, kwani uchunguzi uliofanywa mwaka 2010 na asasi moja iitwayo Uwazi ulidhihirisha kuwa kwa kila kodi ya shilingi moja inayokusanya serikali inatumia shilingi karibu mbili. Kila mmoja anaelewa kuwa kutumia zaidi ya kile unachopata maana yake utamtegemea jirani au mjomba au utageuka ombaomba. Na serikali halikadhalika.

Kinachofanyika ni kuwa Serikali inaposhindwa kukusanya kodi, kwa kawaida hukopa kutoka vyanzo vya ndani, kama Benki Kuu, benki binafsi, kampuni za bima, mifuko ya pensheni, watu binafsi na kadhalika.

Serikali hukopa ndani ya nchi kwa kuuza hatifungati au dhamana kupitia Benki Kuu.

Hili ni deni la ndani ambalo mnamo Septemba 2008 lilikuwa shilingi bilioni 606. Ikumbukwe kuwa sehemu kubwa ya deni hili hukopwa ili kulipa deni la zamani pamoja na riba.

Pili, mikopo hii aghlabu ni mbadala ya kodi isiyokusanywa. Ni mkopo wa kuendeshea Serikali na wala si kwa kuwekeza katika miradi ya maendeleo.Ni njia ya mkato badala ya kukusanya kodi. Na kama alivyopata kunena Mwalimu Nyerere, serikali corrupt haikusanyi kodi

Ukiacha deni la ndani kuna deni la nje. Kuna “wahisani” ambao tunawategemea kwa ruzuku ili kufidia nakisi katika Bajeti ya Serikali. Mwaka jana Sh. 3.8 trilioni ziliahidiwa na wahisani lakini kilichopatikana ni asilimia 29. Ndipo tunapolazimika kukopa.

Ukweli ni kuwa “mfadhili” akitaka anatoa akitaka anazuia. Serikali inayotegemea misaada ya nje inalazimishwa kutimiza masharti ya hao wanaojiita wafadili. Matokeo yake tunakuwa na serikali inayowajibika kwa wahisani badala ya kwa wananchi

Tukiacha deni hilo la hivi sasa la dola bilioni 17.10 alilozungumzia Mkuya, tukirudi nyuma tunaona kuwa mwaka 1970 deni letu lilikuwa dola bilioni 1.45 na likaongezeka hadi dola bilioni 7.9 mnamo 1998. Desemba 2006 ikawa dola bilioni 7, na Januari 2009 lilikuwa dola bilioni 7.8 na Julai 2010 ikawa bilioni 10. Hii inatupa picha jinsi deni linavyokua kila mwaka.

Ni mzigo mkubwa unaoendelea kuongezeka kwa sababu tunaendelea kuongeza deni na papo hapo riba inaendelea kuongezeka.

Kwa mfano, Desemba 2012 tulilipa madeni ya dola milioni 19. Kati ya hizi milioni nne ni deni halisi na milioni mbili ni riba.

Kimsingi, kukopa si kitu kibaya. Swali muhimu ni kujiuliza tunakopa kwa ajili ya nini? Serikali inadai tunatumia mkopo kwa ajili ya sekta za kijamii. Lakini fedha hizi zinatumika ili kuziba pengo au nakisi katika bajeti ya serikali.

Serikali inashindwa kukusanya kodi ya kutosha au labda kodi inayokusanywa inapotea. Matokeo yake inalazimika kukopa ili kuendesha mambo yake. Baya zaidi, ni kuwa sehemu kubwa ya mikopo inaishia mifukoni mwa mafisadi na wajanja wachache. Wanafaidika wachache na mzigo wa deni unabebwa na wananchi wote.

Mfano mmoja ni yale malipo ya pembejeo kwa wakulima, fedha ambazo tulizikopa kutoka Benki ya Dunia (WB). Ni mkopo wa shilingi bilioni 574 ambao ulitumika vibaya na sasa Serikali inajipanga upya kwenda kukopa tena. Benki ya Dunia inasema asilimia 60 ya bajeti ya pembejeo ililiwa na mafisadi.

Kwa mfano, katika Kijiji cha Lunyala, wilayani Nkasi, asilimia 70 ya wananchi walioorodheshwa kupata mbolea walikuwa bandia.

Chini ya mradi huu, serikali hulipia shilingi 140,000 kupitia vocha anazopewa mkulima na kuziwasilisha kwa mawakala wa mbolea na mbegu. Hivyo mkulima hulipia shilingi 80,000 tu.

Serikali kupitia Wizara ya Kilimo na Chakula hutengeneza vocha hizo na kuzigawa vijijini. Serikali ya kijiji huwapa wakulima wake vocha. Wao huipeleka kwa mawakala wa pembejeo. Wanalipa fedha ya juu na kupewa mbolea na mbegu. Mawakala hupeleka fedha hizi NMB ambayo huwalipa mawakala fedha ya thamani ya vocha.

Kisha Wizara ya Fedha nayo huilipa NMB. Kwa ujumla Serikali imetumia jumla ya shilingi 574 bilioni katika mradi huu. Sehemu ya fedha hizi ni mkopo wa dola 160 milioni kutoka Benki ya Dunia.

Mfumo mzima umegundulika kuwa na ufisadi ambapo orodha ya wafaidika huchakachuliwa kiasi cha kuweka hata watu waliokufa kwamba wamepokea mbolea. Mawakala walikuwa wananunua vocha kutoka kwa wakulima kwa shilingi 10,000 au hata kwa shilingi 2,000 na wao kwenda kulipwa shilingi 140,000 benki kana kwamba waliuza mbolea ile kwa wakulima kumbe hakuna mbolea yoyote aliyopewa mkulima.

Inasemekana asilimia 60 hadi 70 ya Bajeti ya Pembejeo ya ruzuku haikufikia walengwa na ilitafunwa na mtandao wa maafisa wa wizara ya kilimo, wakuu wa wilaya, makampuni ya mbolea na mawakala wa pembejeo. Hatuambiwi kama kuna hatua za kisheria zimechukuliwa.

Hivi ndivyo mikopo ya serikali inavyotumiwa. Mara nyingi miradi inayoanzishwa kwa mikopo inashindwa kujiendesha. Kinachosikitisha zaidi ni tabia ya serikali kukopa kwa lengo la kuendeleza matumizi yake makubwa yasiyo ya lazima.

Haifiki wiki moja tunasikia kiongozi wa kitaifa amesafiri nje ya nchi huku akifuatana na msururu wa mawaziri, wapambe na maofisa wanaotafuna posho zisizoeleweka. Hata safari za ndani nazo ni za matanuzi. Misafara mingi inakuwa na mashangingi yasiyopungua 30.

Kuna wanaosema kuwa nchi yetu sasa inakopesheka kwa sababu tumeanza kuzalisha gesi kwa wingi ambayo itatuongezea utajiri mkubwa, hivyo tutaweza kuhimili madeni.

Hii ni ndoto. Tumekuwa tukizalisha dhahabu kwa maelfu ya tani mpaka sana lakini tungali tumeelemewa na madeni. Ndivyo ilivyo katika dhahabu na almasi na ndivyo inavyoweza ikawa katika gesi.

Ndiyo maana mkurugenzi wa Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) wa Kanda ya Afrika, Dak Roger Nord, alitamka kuwa ingawa uchumi wa Tanzania umekuwa ukikuwa kila mwaka lakini wanaofaidika ni matajiri kuliko masikini.

Ni dhahiri kuwa tunahitaji mjadala mpana wa kitaifa kuhusu deni la Taifa ili kujua uhalali wa deni na matumizi yake.

Kwani suala si kukopa bali unakopa kwa ajili ya nini, na hicho unachokopa unakitumiaje. Haiwezekani serikali ikope kisha fedha ziliwe na wachache, halafu deni lilipwe na wajukuu wetu bila ya kuona hizo fedha zilivyotumika.

Deni la Taifa limekua kwa kasi ya kutisha kutoka shilingi 10 trilioni mwaka 2005 hadi shilingi 27 trilioni mwishoni mwa mwaka jana.

Kuna uwezekano wa kuongezeka kwa deni hilo hadi kufikia shilingi 30 trilioni mwaka ujao iwapo kutakosekana utashi wa kukabiliana na hali hiyo, iwapo matumizi ya serikali yataongezeka kuliko mapato, na iwapo matanuzi yataendelea.

Hivi ndivyo ilivyo, kwani nakisi ya bajeti ya serikali imeongezeka kutoka shilingi 389 bilioni mwaka 2007/08 sawa na asilimia 1.7 ya Pato la Taifa na kufikia shilingi 2992 bilioni mwaka 2012/13 sawa na asilimia 6.2 ya Pato la Taifa.

Mwaka huu 2013/14 hali ni mbaya kwani bajeti imefumuka, mapato ni madogo kuliko makadirio na matumizi yamekuwa makubwa.

Matumizi makubwa ni ya kulipa madeni pamoja na riba. Tutatumia shilingi trilioni 2.3 kwa madhumuni haya. Itafika wakati matumizi haya yatakuwa zaidi ya matumizi ya afya, maji na elimu. Hali inatisha.source

Matumizi makubwa ni ya kulipa madeni pamoja na riba. Tutatumia shilingi trilioni 2.3 kwa madhumuni haya. Itafika wakati matumizi haya yatakuwa zaidi ya matumizi ya afya, maji na elimu. Hali inatisha.
- See more at: http://raiamwema.co.tz/deni-la-taifa-laongezeka-kwa-kasi-kutokana-na-matanuzi#sthash.wvIxrpoI.dpuf

Post a Comment

CodeNirvana
© Copyright WORLD OF TODAY Published.. Blogger Templates
Back To Top