OVYO: Moyes akiri hali ni mbaya Old Trafford













HALI ni mbaya zaidi. Mtu anayesakamwa zaidi katika mchezo wa soka kwa sasa, kocha David Moyes wa Manchester United, amekiri kuwa hali ni mbaya sana Old Trafford kuliko wakati mwingine wowote.


Wakati mashabiki wa timu hiyo wakiamini kuwa timu yao ilikuwa imeshinda 2-1 katika pambano dhidi ya Fulham juzi Jumapili, katika sekunde za majeruhi, mshambuliaji wa Fulham, Darren Bent, alifunga bao lililoipatia sare ya 2-2 timu yake katika dimba la Old Trafford.


Bao hilo limeiacha Manchester United ikiwa pointi tisa nyuma ya timu inayoshika nafasi ya nne, Liverpool, ambayo saa 24 kabla ya mechi hiyo ilikuwa imeiburuta Arsenal mabao 5-1 katika Uwanja wa Anfield.


Alipoulizwa kama alijua kuwa mambo yangekuwa kama yalivyo sasa, Moyes alijibu: “Hapana kwa kweli. Imekuwa kama hivi msimu huu, lakini leo (juzi Jumapili) imekuwa mbaya mno. Unaweza kusema kwamba tulikuwa laini sana akilini na hatukumaliza kazi yetu. Nakubali.


“Tulitawala mchezo. Kufungwa bao moja lilikuwa jambo baya. Kiasi cha nafasi tulizotengeneza, tulizojaribu na jinsi tulivyocheza ilishangaza sana kwa nini hatukushinda, yaani sielewi.


“Tulimiliki mpira kadiri tulivyoweza. Tungeweza kufunga zaidi. Wachezaji walijaribu na mabao yalikuja, hata wakati walipofungwa 2-1 na dakika tano kuongezwa Fulham bado hawakucheza vizuri, walituacha sana na mpira kwa hiyo lilikuwa suala la kupoteza muda, lakini ghafla tukawapa bao la kijinga sana.


“Wachezaji wameumia sana. Naona kila siku jinsi wanavyoumizwa kwa sababu matokeo hayaji kama wanavyotaka. Lakini tuna timu nzuri na kuna timu chache sana zinazotamani kucheza na sisi, nina uhakika.”


Kwa mara ya kwanza baada ya miaka mingi, Manchester United sasa iko katika hatari ya kukosa nafasi ya kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya na Moyes alipoulizwa kuhusu suala hilo, alijibu kwa kifupi: “Tutajaribu kadiri tuwezavyo.” Beki wa zamani wa Liverpool, Jamie Carragher, ambaye kwa sasa ni mchambuzi mahiri wa soka England, alikiri kwamba hajawahi kuona timu inajihami kwa kiasi kile kama ambavyo Fulham ilifanya katika mechi dhidi ya Manchester United

Post a Comment

CodeNirvana
© Copyright WORLD OF TODAY Published.. Blogger Templates
Back To Top