. 
MAMLAKA ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetoa tahadhari ya kuwapo mvua kubwa na upepo mkali katika wiki hii.
Taarifa hiyo imetaja maeneo yatakayoathirika kuwa ni mikoa ya iliyo karibu na pwani ya Bahari ya Hindi pamoja na baadhi ya mikoa ya kusini.
Katika taarifa yake, TMA imesema kutakuwa na vipindi vya mvua kubwa (zaidi ya mm 50 ndani ya saa 24) kati ya Jumatano na Alhamisi wiki hii.
Aidha, taarifa hiyo imeeleza kwamba kutakuwa na upepo mkali unaozidi kilomita 40 kwa saa, pamoja na mawimbi makubwa zaidi ya mita 2.0.
Maeneo yaliyotajwa kuweza kuathiriwa na hali hiyo ni ukanda wa pwani mikoa ya Tanga, Dar es Salaam, Pwani, Lindi, Mtwara pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba, Mbeya, Njombe, Ruvuma pamoja na kusini mwa mkoa wa Morogoro.
Imeelezwa kwamba hali hii inatokana na kuwepo kwa kimbunga “FOBANE” kusini magharibi mwa Bahari ya Hindi.
“Mfumo huu unatarajiwa kuvuta upepo kutoka Pwani ya Somalia na misitu ya Congo kuelekea maeneo ya nchi yetu. Watumiaji wa Bahari na wakazi wa maeneo hatarishi wanashauriwa kuchukua tahadhari,” imeeleza TMA kupitia taarifa yake hiyo. Soma zaid

Post a Comment