
Kasisi mmoja raia wa Australia
amefichua na kuthibitisha kuwa kuna idadi kubwa ya wafungwa wenye asili
ya Afrika katika magereza ya Hong Kong, wengi wao wakiwa ni kutoka
Tanzania.
Kasisi huyo John Wortherspoon ambaye kwa sasa anafanya
ziara maalum Tanzania, amesema yeye ndiye ambaye amekuwa akisambaza
barua zinazodaiwa kuandikwa na wafungwa wanaoshikiliwa kwenye magereza
hayo ambapo baadhi yao wametaja majina ya watu wanaodaiwa kuwa
wafanyabiashara wakubwa wa dawa za kulevya waliowatuma kusafirisha dawa
hizo.
Padre Wotherspoon amefika kuonana na familia za wafungwa hao
pamoja na idara za serikali zinazohusika na mapambano dhidi ya biashara
hiyo hatari ya dawa za kulevya. Mwandishi wetu Ben Mwang'onda
anasimulia zaidi kutoka Dar Es Salaam BBC
Post a Comment