Bryson Nyeregete
CHAMA
cha Mapinduzi (CCM) Mvomero Morogoro, jana kimeonesha kutetemeshwa na
M4C ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema na Oporesheni Pamoja
Daima (OPD), ambapo serikali na viongozi wa CCM wilayani, wamelazimika
kuwapiga Changa la Macho wakulima na wafanyakazi wa kiwanda cha Sukari
Mtibwa.
Katika
kuweweseka huko, Viongozi wa Serikali na CCM wilayani, imewalazimika
kusimamisha kwa muda uzalishaji wa Sukari Mtibwa, hadi kitakapowalipa
wafanyakazi, wastaafu na wakulima wadogo wa miwa, jambo ambalo imedaiwa
ni kiini macho, M4C-OPD ikipita, dhuluma zitaendelea.
Tangu
kubinafsishwa kwa kiwanda hicho kwa mwekezaji huyo kwa bei poa,
wameshafika Mawziri 20 wakiwemo mawaziri wakuu watatu hadi sasa na Rais
Jakaya Kikwete, lakini hakuna aliyetatua ucheleweshwaji wa malipo na
dhuluma kwa wakulima na wafanyakazi, huku kesi Lukuki zikiwa mahakamani.
“Ni
mbinu za Nguruwe kujiosha matope awe mbele ya watu na baadaye
kuyarejea. Wakulima na wafanyakazi tumebaini tumepigwa Changa la Macho,
ili kupumbazwa wakati Chadema watakapomwaga sera zao, CCM na viongozi wa
Serikali waonekane wameshughulikia kero zetu.
“Mwekezaji
wa Mtibwa amekuwa kama Sikio la Kufa halisikii Dawa kutokana na kiwanda
kumilikiwa na Mabosi wa CCM na Serikali, ambapo kila mmoja ana mizizi
yake hapo, hivyo hakuna wa kumfunga paka Kengele, maana kesi ya Nyani
hawezi kuhukumu Tumbili”alisema mkulima mmoja.
Katika
Kikao cha Wakulima na Wafanyakazi, kilichofanywa jana, Mkuu wa Wilaya,
Antony Mtaka, kabla ya kufunga uzalishaji kwa muda, Meneja wa Kiwanda
hicho Yahya, aliwahadaa wakulima kuwa malipo yao zaidi ya Sh. Bil. 1/-
na malipo ya wafanyakazi Mil 200/- yatalipwa Februari, 2014.
Aidha
mmoja wa Viongozi wa Chadema atakayetua na Chopa kiwandani hapo na
kutaka jina lake lisitajwe alisema, Chadema M4C-OPD, tayari inazo
taarifa za kiinterejensia kuhusu change la macho kwa wakulima na
wafanyakazi wa mtibwa, na kudai waichague chadema imalize Uhuni na
Usanii wa CCM na viongozi wake, na ikibidi kuwafikisha wahusika
mahakamani.
“Walikolalia
CCM sisi Chadema tumeamkia huko. Tuna taarifa, wafanyakazi wastaafu
zaidi ya 110 wamekufa bila kupata mafao yao, na waliopata malipo yao
yamechakachuliwa hayafiki hata Mil. 2/-; Ingawa mfanyakazi amefanya kazi
zaidi ya miaka 30, fedha ya makato yao yote anayo mwekezaji kwenye
Akaunti yake”.alisema.
Post a Comment