Ambaka mama yake mzazi, dada zake wawili na majirani


Musoma. Wakati leo ni Siku ya Mama Duniani, kijana mmoja wa mjini hapa, anashikiliwa na polisi kwa tuhuma za kumbaka mama yake mzazi, dada zake wawili na wanawake wengine wawili jirani wa familia yao.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara, Ramadhan Ng’anzi alisema jana kwamba tukio hilo lilitokea Jumanne iliyopita saa 10 alasiri wakati mama wa kijana huyo alipofika nyumbani kutoka kazini akiwa na mtoto wake wa kike.

Akisimulia mkasa huo, Ng’anzi alisema baada ya mama huyo kufika nyumbani na mtoto hao, kijana huyo alimvamia na kumbaka huku rafiki yake (rafiki wa mbakaji) akilinda mlango wa kutokea ili kuwazuia wasitoke.

“Vijana wengine marafiki wa kijana huyo walikuwa kwenye geti wakilinda ili kuwazuia walioko ndani wasitoroke,” alisema Kamanda.

Kamanda alisema kijana huyo mbakaji alipomaliza kumtendea mama na dada zake unyama huo alimwamuru mama yake mzazi kuwapigia simu marafiki zake ili wafike nyumbani hapo na walipofika kijana wa mama huyo aliwateka huku akiwatishia kwa panga na kuwabaka kwa kuwaingilia kinyume na maumbile.

Alisema baada ya kumaliza kuwafanyia ukatili huo, aliwapiga picha wanawake hao wakiwa uchi kwa kutumia simu yake ya mkononi na kisha kuwaamuru kuondoka katika nyumba hiyo bila kelele.

“Pia aliwatisha kwa kuwaambia wasithubutu kusema popote kitendo alichowafanyia na endapo watafanya hivyo aliwaambia atawaua,” alisema Kamanda Ng’anzi

Alisema baada ya kijana huyo na kundi lake kuwaachia wanawake hao walikimbilia nyumbani za jirani na kutoa taarifa.

Baada ya taarifa hizo, majirani walijikusanya na kwenda kumvamia kijana huyo wakiwa na silaha za jadi sambamba na kutoa taarifa polisi.

“Polisi walifika eneo la tukio na kuwakuta wananchi wakiwa wamewakamata vijana hao wawili na tayari walikuwa wamejeruhiwa vibaya, hivyo wapo katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa kwa ajili ya matibabu lakini wakiwa chini ya ulinzi wa polisi na watafikishwa mahakamani wakati wowote” alisema Kamanda.

Mama azungumza

Akizungumzia tukio hilo, mama mzazi wa kijana huyo huku akibubujikwa na machozi alirejea kile kilichosemwa na Kamanda Ng’anzi kwamba alibakwa na kuamuriwa kuwaita kwa simu majirani zake.

Wanawake wengine waliobakwa walisema kitendo walichofanyiwa na kijana huyo ni cha kinyama, hakivumiliki katika jamii na kwamba walichofanyiwa ni aibu kusimulia katika vyombo vya habari.

“Mimi nilipigiwa simu na mama yake mzazi kuwa niende kwake mara moja kuna kitu anataka anieleze, nami nikaenda kuingia sebuleni namkuta yupo na kijana wake, binti na kijana mwingine, ghafla akaja huyu mwenzangu, tukashangaa tunaamriwa kwa panga ingieni humu, tukaingia na kuanza kufanyiwa ukatili,” alisema mama huyo aliyefanyiwa unyama.

Majirani wamzungumzia mbakaji

Wakizungumzia tukio hilo, majirani Doto Ochayo na Pendo Elias walisema kijana huyo ni kibaka mzoefu na kuwa hiyo si mara ya kwanza kumbaka mama yake. Pia, walisema kwamba alishawahi kufungwa jela miaka 15 na ametoka hivi karibuni.

Ukubwa wa tatizo

Juzi, bungeni mjini Dodoma, Waziri wa Katiba na Sheria, Dk Harrison Mwakyembe alisema hadi Machi, mashauri ya ubakaji na ulawiti yaliyokuwa mahakamani ni 2,031 huku takwimu zikionyesha kuwa kila siku watu 19 hubakwa na kulawitiwa.

Hali hiyo ni sawa na watu 570 wanaobakwa au kulawitiwa kwa mwezi au watu 6,840 kwa mwaka.

Ripoti iliyotolewa hivi karibuni na Chama cha Wanahabari Wanawake Tanzania (Tamwa) inadai kuna ucheleweshaji na upotoshwaji wa ushahidi wa kesi za vitendo vya ukatili wa kijinsia hasa ubakaji na ulawiti katika ngazi ya Mahakama, polisi na baadhi ya madaktari hospitalini.

Tamwa ilibainisha kuwa jumla ya kesi 62 za ubakaji zimeshindwa kutolewa hukumu au uamuzi na Mahakama mbalimbali jijini Dar es Salaam katika kipindi cha 2014 hadi 2015.

Taarifa hiyo ilibainisha kuwa ni kesi moja tu ambayo mtuhumiwa alihukumiwa kifungo cha miaka 30 jela, kesi 43 bado ziko mahakamani huku kesi 17 hazijafishwa mahakamani.

Mwanasiasa mkongwe nchini, Anna Abdallah alisema kushamiri kwa matukio hayo kunachangiwa na kuongezeka kwa kasi mmomonyoko wa maadili nchini.

Alisema katika baadhi ya maeneo, matukio ya ubakaji na ulawiti yanafanywa na ndugu kwa kusukumwa na imani za kishirikina chanzo mwananchi

RATIBA YA USAILI WA MITIHANI YA MCHUJO WA KADA ZA MJNUAT UTAKAOFANYIKA CHUO KISHIRIKISHI CHA ELIMU DAR ES SALAAM (DUCE) TAREHE 05/03/2016

   see more
AWAMU YA PILI: SAA TATU NA NUSU ASUBUHI
UKUMBI
KADA
LECTURE THEATRE  “A”
Ø  PROCUREMENT AND SUPPLIES OFFICER II             
LECTURE THEATRE  “B”
Ø  ASS.  PROCUREMENT AND SUPPLIES OFFICER II 
Ø  PUBLIC RELATION OFFICER II       
LECTURE THEATRE  “C”
Ø  INTERNAL AUDITOR II      
Ø  OFFICE ASSISTANT         

MATOKEO YA UWALIMU 2015 (DIPLOMA) BOFYA HAPA KUFUNGUA

 
Baraza la Mitihani nchini Necta leo limetangaza matokeo ya mitihani ya uwalimu nakidato cha sita na kusema kuwa umefaulu umeongezeka kwa asilimia Matokeo ya diploma ya uwalimu bofya hapa

Kaburi la aliyezikwa na kuku lafukuliwa , CHEKI PICHA HAPA





KABURI la Bernadetha Steven (35) aliyefariki na kudaiwa kuzikwa na kifaranga cha kuku tumboni wiki iliyopita katika mtaa wa Masekelo katika kata ya Masekelo, Manispaa ya Shinyanga, limefukuliwa na watu wasiojulikana.

Mkuu wa Upelelezi wa Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga, Mussa Taibu amethibitisha kuwapo kwa tukio hilo, huku akisema tukio hilo halivumiliki na kuwataka wananchi kushirikiana na Jeshi la Polisi kufanya uchunguzi wa wahusika wa tukio hilo.

Taarifa za kufukuliwa kwa kaburi hilo zilianza kusambaa juzi majira ya saa 1:00 usiku ambapo jana asubuhi viongozi wa eneo husika pamoja na aliyekuwa mume wa marehemu, Deo Masanja walifika eneo la tukio na kukuta kaburi limefukuliwa huku nyayo za miguu ya watu ikionekana karibu na kaburi hilo hali iliyowatia hofu kubwa.

Mjumbe wa Serikali za Mitaa wa Mtaa wa Masekelo, Josephine Kishiwa aliwaeleza waandishi wa habari kuwa alipata taarifa za tukio hilo baada ya kuelezwa na baadhi ya wananchi na kuamua kuwatafuta viongozi wenzake ili kuweza kutatua tatizo hilo.

“Tukio hili ni mara ya kwanza kutokea katika makaburi haya hatujawahi kukuta kaburi limefukuliwa, hiki kitendo kimetusikitisha tunaomba Jeshi la Polisi lifanye uchunguzi wa kina ili tujue chanzo cha tukio hili,” alisema Kishiwa.

Bernadetha alifariki dunia Juni Mosi mwaka huu na kuzikwa siku mbili baadaye ambapo wakati wa maziko yake inadaiwa ndugu wa marehemu walifanya tambiko kwa kuchana tumbo la marehemu na kuweka kifaranga cha kuku kilichochinjwa wakidai wanaondoa mikosi ili mtu mwingine asiugue ugonjwa uliomuua ndugu yao huyo, ingawa hata hivyo haikuelezwa ni ugonjwa gani.  Habari leo
Older Posts
© Copyright WORLD OF TODAY Published.. Blogger Templates
Back To Top