FIFA YAWATIA KIFUNGONI NYOTA WANNE

 



 



Rio de Janeiro, Brazil. Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa) limetangaza kuwatia kifungoni nyota wanne ambao watazikosa mechi kadhaa za fainali za Kombe la Dunia mwaka huu.


Nyota hao wanatoka mataifa tofauti matatu na wametiwa kifungoni kwa sababu mbalimbali zikiwamo za kuonyeshwa kadi nyekundu katika mechi za kufuzu kwa fainali hizo.


Miongoni mwao ni nyota wa Croatia, Mario Mandzukic anayeichezea Bayern Munich ya Ujerumani.


Watatu kati yao watakosa mechi za ufunguzi za fainali hizo, huku mmoja akikosa fainali nzima.


Wengine ni kiungo wa Colombia, Fredy Gaurin na mchezaji wa Iran, Sosha Makani.


Pia, yumo mchezaji wa Croatia, Josip Simunic, ambaye kwa upande wake atazikosa fainali hizo baada ya kufungiwa mechi 10 kwa kutoa kauli ya kisiasa wakati wa mchezo baina ya Croatia na Iceland mjini Zagreb, Croatia, mwezi Novemba.


Mandzukic ataikosa mechi ya ufunguzi wa michuano hiyo ya nchi yake dhidi ya wenyeji Brazil mjini Sao Paulo huku Guarin ambaye anaichezea Inter Milan ya Italia akiikosa mechi dhidi ya Ugiriki mjini Belo Horizonte.Chanzo...

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright WORLD OF TODAY Published.. Blogger Templates
Back To Top