HIVI NDO VITIMBWI KATIKA BUNGE LA KATIBA, Soma kwa undani zaidi.

 









Dar es Salaam. Bunge Maalumu la Katiba mapema wiki hii lilianza safari yake ya siku 70, kujadili Rasimu ya Pili ya Mabadiliko ya Katiba kwa lengo la kuiboresha, kabla haijapelekwa kwa jamii kwa ajili ya kura ya maoni.


Katika siku za mwanzo za Bunge hilo linalofanyika mjini Dodoma, mambo kadhaa yameibuka na kuzua gumzo ndani na nje ya ukumbi wa Bunge.


Mume na mke ndani ya Bunge


Katika hali isiyokuwa ya kawaida na iliyovuta hisia za wengi ni kuwapo kwa watu wawili miongoni mwa wajumbe wa bunge hilo ambao ni mtu na mkewe.


Wajumbe hao ni Dk Emmanuel Makaidi ambaye ni mwenyekiti wa Chama cha National League for Democracy (NLD) na mke wake, Modesta Ponera ambaye ni mwanachama wa chama hicho.


Kitendo hicho kimelalamikiwa na baadhi ya wananchama wa chama hicho, hasa wale wa Zanzibar, ambao walimtaka Rais Jakaya Kikwete kufuta uteuzi wa wajumbe hao kwa madai kuwa walioteuliwa katika chama hicho ni mtu na mkewe na kufanya uteuzi huo kukosa sura ya muungano.


Dk Makaidi alikiri kuwa Ponera ni mke wake, lakini akasema ni mwanachama wa NLD, hivyo ana haki ya kuteuliwa kama mjumbe mwingine yeyote na kwamba kuwa mkewe kamwe hakumwondolei sifa za kuchaguliwa kuwa mjumbe wa bunge hilo.


‘Walilia nyongeza ya posho’


Hali ya ubinafsi na msemo wa Kiswahili wa aliyeshiba hamjui mwenye njaa ilijitokeza siku chache baada ya Bunge Maalum la Katiba kuanza mjini Dodoma.


Imekuwa kawaida kwa wananchi wanaposikia kuwa wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wakiomba kuongezewa posho hulalama kuwa wanajineemesha wao na kuwaacha wapigakura wao wakisota kwa ugumu wa maisha.


Wakijadili rasimu ya kanuni za bunge, wajumbe kadhaa walitaka waongezewe posho kwa kile walichodai ni kupanda kwa gharama za maisha tangu kuanza kwa mkutano huo. Wajumbe hao waliomba kiwango wanachppewa sasa cha Sh 300,000 kwa siku kiongezwe kwa kuwa hakiwatoshi, hivyo wakapendekeza kiongezwe ili kiweze kukidhi mahitaji muhimu som zaid

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright WORLD OF TODAY Published.. Blogger Templates
Back To Top