
Dar es Salaam. Kauli ya Rais Jakaya Kikwete ya
kuwataka wanachama, wadau na makada wa CCM, kuondokana na unyonge,
imepokewa kwa hisia tofauti huku ikielezwa kuwa ni ya vitisho.
Juzi, wakati akifungua Mkutano wa Halmashauri Kuu
ya CCM mjini Dodoma, Rais Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa chama
hicho tawala alisema: “Ni wakati wa kuacha unyonge na uvumilivu una
kikomo chake.”
Alisema CCM inaingia kwenye uchaguzi huku
ikishindana na wagomvi: “...Ugomvi ndiyo sehemu ya mwongozo wao kufanya
siasa,” alisema Kikwete bila kutaja jina la chama chochote cha siasa.
Alisema amechoshwa na vitendo vya ugomvi huku
akitolea mfano wa tukio la Kahama mkoani Shinyanga ambako kijana mmoja
alitolewa macho kwa bisibisi na mwingine kumwagiwa tindikali katika
uchaguzi mdogo wa ubunge Igunga, mkoani Tabora.
Akizungumza kwa simu jana, Mwenyekiti wa Chadema,
Freeman Mbowe alieleza kushangazwa kwake na kauli ya Rais Kikwete
akisema: “Nimeipokea kwa mshtuko na ninawataka wafuasi wa chama changu
kuwa watulivu na kuchukua tahadhari kubwa.”
“Nilichokifanya ni kuwaagiza wafuasi wa Chadema
kufanya kampeni za kistaarabu kwa kutolipiza kisasi ili kuhakikisha
kwamba hakuna damu ya Mtanzania itakayomwagika Kalenga,” alisema.
Hatua ya Rais Kikwete, imekuja baada ya CCM
kumtangaza, Godfrey Mgimwa kuwa mgombea ubunge wa Jimbo la Kalenga.
Mgimwa ni mtoto wa aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo, ambaye pia alikuwa
Waziri wa Fedha, hayati Dk William Mgimwa aliyefariki mwezi uliopita
nchini Afrika Kusini.
Mgombea huyo atachuana na mgombea wa Chadema, Grace Tengega.
Jana, Mbowe alisema ingawa Kikwete ni Mwenyekiti
wa CCM, alitakiwa kufahamu kwamba ni kiongozi wa nchi na ni Amiri Jeshi
Mkuu ambaye vikosi vya Ulinzi na Usalama vipo chini yake.
“Anapotoa kauli nzito kama hiyo, inatakiwa afahamu
kwamba yeye si Mwenyekiti wa CCM tu, bali ni Rais na Amiri Jeshi Mkuu,
hakustahili kutoa kauli kama hiyo inayoweza kuamsha hisia,” alisema
Mbowe.
Alisema kauli zake za kiitikadi za kupendelea
chama chake wakati akifahamu kuwa yeye ni kiongozi wa Watanzania wote,
zinawafanya wananchi wagawanyike kwa misingi ya vyama.
“Rais Kikwete anadai kwamba mtu wao alimwagiwa
tindikali na mwingine kutolewa macho kwa bisibisi, lakini hazungumzii
viongozi na wanachama wa Chadema waliouawa kwa kupigwa risasi na wengine
kwa mabomu. Anasema hayo huku akifahamu fika kwamba kuna vyombo vya
dola na Mahakama ambavyo vinashughulikia matukio hayo Soma zaidi...........
Post a Comment