NINI HATIMA YA KESI YA KENYATTA ICC?







Rais Kenyatta na wakili wa Naibu Rais William Ruto Karim Khan


Pande zinazohusika katika kesi inayomkabili Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta kwenye mahakama ya kimataifa ya ICC Mjini The Hague zimekuwa na kikao cha kujadili mstakabali wa kesi hiyo.

Kiongozi wa mashtaka wa ICC Fatou Bensouda amekiri kuwa bado hana ushahidi wa kutosha kuwezesha kesi hiyo kuendelea.




wanataka kesi hiyo kuhusiana na ghasia za baada ya uchaguzi wa Kenya mwaka 2007 itupiliwe mbali.

Bensouda amesema kuwa bado kuna maswala yanayozua utata na ambayo yanahitaji uchunguzi wa kina.

Mawakili wa Kenyatta wanatuhumu upande wa mashitaka kwa kusisitiza kutaka taarifa kuhusu akaunti ya benki ya Rais Kenyatta kuona ikiwa kuna pesa zozote zilizotolewa kwa lengo la kutumika wakati wa ghasia za baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2007/08

Wakili wa waathiriwa mesisitizia mahakama kuwa kutupiliwa mbali kwa kesi kuwakosesha waathiriwa haki. Mahakama inatarajiwa kutoa uamuzi katika siku chache zijazo.
ICC na Afrika

Mataifa ya Afrika yamekuwa yakikosoa ICC kwa kulenga tu viongozi wa Afrika.

Kesi dhidi ya Kenyatta ni muhimu kwa ICC ambayo imefanikiwa tu kumhukumu mtu mmoja huku nyingi ya kesi zinazofikishwa katika mahakama hiyo zikitupiliwa mbali kutokana na sababu nyingi tu tangu kubuniwa miaka 11 iliyopita.

Wadadisi wanasema kuwa huenda kesi hiyo ikaleta msukosuko katika kanda ya Afrika Mashariki ikiwa viongozi wa mashitaka watasisitiza iendelee.

Rais Kenyatta alifikishwa ICC kutokana na tuhuma kuwa alikuwa mmoja wa washukiwa wakuu wa ghasia za baada ya uchaguzi mkuu nchini Kenya mwaka 2007/2008. Anakabiliwa na makosa ya mauaji na uhalifu mwingine dhidi ya binadamu.

Kadhalika Kenyatta alishitakiwa pamoja na makamu wake wa Rais William Ruto kwa tuhuma sawa. Kesi dhidi ya Ruto inaendelea katika mahakama hiyo.

Mataifa ya Magharibi ambayo yanajitolea katika kuunga mkono ICC, pia yana wasiwasi kuhusu uhusiano wao na Kenya ambayo inaonekana kama mshirika mkubwa katika vita dhidi ya kundi la wanamgambo la Al Shabaab nchini Somalia.

Watu 1,200 walipoteza maisha yao katika ghasia za uchaguzi mkuu mwaka 2007/08 huku maelfu wakilazimika kutoroka makwao. Wote wamekanusha mashitaka.

Viongozi wa mashitaka ICC wanasema kuwa Kenyatta aliongoza ghasia hizo lakini kesi dhidi yake imefanywa dhaifu kutokana na baadhi ya mashahidi kujiondoa katika kesi hiyo tangu kesi hiyo kuwasilishwa katika mahakama hiyo miaka minne iliyopita.

Kesi yenyewe ilitarajiwa kuanza Jumatano, lakini ikaahirishwa kwa mara ya nne mwezi jana wakati ambapo wendesha mashitaka waliposema kuwa shahidi mwingine alijiondoa kwenye kesi huku wakiomba mahakama kuwapa muda zaidi kutafuta ushahidi.

Viongozi wa mashitaka wanasema kuwa mashahidi wengi wamehongwa au kutishwa kiasi cha kujiondoa katika kesi hiyo.

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright WORLD OF TODAY Published.. Blogger Templates
Back To Top