
Dar/Iringa. Inawezekana kuwa baadhi ya wazazi mkoani Iringa, wanamuunga mkono kwa vitendo mwanafalsafa na mwandishi maarufu wa Marekani, Benjamin Franklin, aliyewahi kusema: “Katika mvinyo kuna hekima, ndani ya bia mna uhuru na ndani ya maji kuna bakteria.”
Ingawa kauli ya Franklin iliishia katika maneno, baadhi ya wazazi wakulima katika vijiji mbalimbali mkoani Iringa, wanautekeleza usemi huo kwa vitendo kwa kuwanywesha pombe za kienyeji watoto wao wadogo wanapokuwa shambani, ili walale usingizi ili wazazi hao wapate nafasi ya kulima bila usumbufu.
Uchunguzi uliofanywa na gazeti hili na kuzungumza na baadhi ya wazazi katika maeneo hayo, umebaini kuwa utamaduni huo umekuwapo kwa miaka mingi mkoani humo.
Baadhi ya wazazi waliozungumza na gazeti hili wanasema kuwa ingawa bado wapo baadhi ya watu wanaoendelea na vitendo hivyo, lakini ukweli ni kwamba tayari vijana wengi wameshapata madhara yatokanayo na pombe hiyo ya utotoni.
Wanaofanya kitendo hicho wanasema kuwa wanapofika shambani kwanza huwatafutia watoto wao eneo zuri la kivuli na kuwatandikia vyema, kabla ya kuwanywesha pombe, kisha ndipo mzazi huanza kulima.
Lameck Kihaga, mkulima katika eneo la Itagutwa, anaeleza kuwa zamani ilikuwa kawaida kwa mzazi kumnywesha mtoto wake kikombe kimoja au viwili vya pombe kama dawa ya usingizi.
Anasema kwamba tabia hiyo imesababisha ongezeko kubwa la wanywaji pombe maarufu aina ya ulanzi au komoni mkoani humo ambao bado ni vijana wadogo na wanafunzi wa shule za msingi na sekondari.
“Naamini kabisa, hawa vijana walevi mitaani leo, wengi wao wamelowea kutokana na tabia ya kunyweshwa pombe wakiwa bado wadogo,” anasema Kihaga.
Kauli ya Serikali
Ofisa Maendeleo ya Jamii, Mkoa wa Iringa, Menrad Dimoso anasema kuwa taarifa za wazazi kuwanywesha watoto wao pombe za kienyeji wakati wa kilimo zimekuwapo muda mrefu mkoani humo, lakini siyo tatizo kubwa.
Anasema kwamba wazazi wengi waliokuwa wakifanya vitendo hivyo walishaacha na wanaoendeleza tabia hiyo ni wachache, hivyo haiwezi kuwa na madhara makubwa kwa jamii.
Kadhalika ziko taarifa kuwa kuwanywesha watoto wadogo pombe huweza kuwasababishia wapate utapiamlo na alipoulizwa Dimoso alisema:soma zaidi...............
Post a Comment