
Dar es Salaam.Watoto hao walipewa majina ya
Eliud na Elikana, walizaliwa Februari 20, mwaka jana mkoani Mbeya wakiwa
wameungana huku mama yao Grace Joel (20) akiwa hana matumaini ya watoto
hao kutenganishwa au kuendelea kuishi.
Grace alikata tamaa zaidi baada ya mume wake Erick
Mwakyusa kumtamkia wazi kuwa hana shida na watoto walemavu kwa kuwa
kwenye familia yao ya kina Mwakyusa hakuna walemavu.
“Nilishangaa, familia yangu kunitelekeza baada ya
kugundua watoto wameungana, mume na familia yake walinitamkia wazi kuwa
hawana shida na watoto walioungana, mume wangu alisema hawezi kuwalea
kwa kuwa kwao hakuna watoto wenye ulemavu wa aina hiyo,” anasema.
“Siyo siri nilisijikia uchungu, sikuamini mume
wangu angeweza kunifanyia hivyo;siyo yeye tu hata familia yao sikudhani
kama wangenigeuka hivyo.
“Hospitali ya Kyela ndiyo iliyonipeleka kwenye
Hospitali ya Rufaa Mbeya ambao nao walivyoona hali ya watoto wangu
wakanishauri kuja Muhimbili.Sikuwa na uwezo wa kufika Muhimbili,
nawashukuru sana madaktari wa Rufaa Mbeya, madaktari wa Muhimbili na
hasa Serikali iliyonifuta machozi.
Leo hii siamini kama ninawashika watoto wangu kila
mmoja akijitegemea, sina cha kuwalipa zaidi nawaombea kwa Mungu wale
wote walionisaidia kwa njia moja ama nyingine.
Kauli ya kukataliwa na mumewe ilikuwa mwiba
mchungu kwa Grace ambaye alihisi dunia yote imemgeuka, na hakuwa na
msaada toka kwa familia ya mume wake na familia yake pia.
Akiwa kwenye hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mbeya,
Grace alikata tamaa kabisa kuwa watoto wake Elikana na Eliud ambao
aliwazaa kwa njia ya operesheni wakiwa na kila tano na nusu, kama
watapona. Muda wote mama huyo alijawa machozi machoni mwake kwa kuamini
watoto wake wasingepona.
Watoto hao walikuwa na njia moja ya kutolea haja ndogo pia njia ya haja kubwa walikuwa wanatumia moja.
Februari 25 mwaka jana, Grace akiwa na watoto wake
ambao alikuwa amewafunika kwa upande mmoja wa kanga, akiwa hana uwezo
hata wa kuwanunuliwa maziwa, alipewa rufaa na kufikia kwenye Hospitali
ya Muhimbili na kulazwa kwenye wodi ya watoto, wakiwa chini ya uangalizi
maalumu.
Daktari Zaituni Bokhari ndiye aliyekuwa
akiwahudumia kwa karibu watoto hao na kumwombea misaada kwa watu
mbalimbali ambao walijitokeza kuwanunulia nguo, maziwa na vitu vingine
vingi.
“Ilikuwa kazi kubwa kumfanyia ushauri Grace hadi
akubaliane na hali halisi, alikuwa amekata tamaa kabisa, ni kama
alichanganyikiwa. Kuna wakati alitaka kutoroka Hospitali na kuwaachaa
watoto, lakini ilibidi tuwe naye karibu na kumpa moyo na kumwambia
watoto wake watapona. Tunashukuru kwamba baadaye akili yake ilitulia soma zaidi..........
Post a Comment