MWENYEKITI wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba ameweka bayana juhudi zilizopata kufanyika kuzima mapendekezo kuhusu muundo wa serikali tatu ndani ya Muungano, licha ya mapendekezo hayo kutolewa na tume kadhaa baada ya utafiti.
Akiwasilisha rasimu ya Katiba mpya, Jaji Warioba alisema mapendekezo hayo yanajumuisha yale yaliyotolewa na Tume za Jaji Francis Nyalali na Jaji Robert Kissanga.
Tume ya Jaji Nyalali
Alisema kati ya mapendekezo kuhusu serikali tatu ambayo hayakufanyiwa kazi ni pamoja na ya Tume ya aliyekuwa Jaji Mkuu, Francis Nyalali.
Alisema Warioba: “Mwaka 1991, Tume ya Jaji Nyalali ilipendekeza muundo wa serikali tatu. Ingawa pendekezo hili halikukubalika, Zanzibar iliamua kuwa na bendera na nembo yake na baadaye sharti likawekwa kwamba meli zinazoingia kwenye bandari za Zanzibar ni lazima zitumie bendera ya taifa yenye nembo ya Zanzibar. Kwa maana nyingine, Zanzibar ikaanza kutumia Bendera ya Taifa iliyo tofauti.
Vuguvugu la Z’bar na OIC
Jaji Warioba alisema mwaka 1992, Zanzibar ilijiunga na Organisation of Islamic Conferece (OIC) na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania lilipitisha Azimio.
Alisema Azimio hilo la Bunge lilikuwa likizitaka serikali zote mbili kushirikiana katika kutafuta ufumbuzi wa tatizo hilo na matatizo mengine ya Muungano na kutoa taarifa bungeni katika kipindi cha mwaka mmoja.
Mfululizo wa kuzima hoja
Alisema mwaka 1993, wakati wa mkutano wa Bunge la Bajeti kwa upande wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, wabunge kutoka Tanzania Bara (G 55) walipeleka bungeni hoja ya kuundwa kwa Serikali ya Tanganyika na hoja hiyo ilipitishwa.
Alisema Novemba mwaka 1993, kikao maalumu cha CCM na serikali zote mbili kilifanyika Dodoma ili kutafuta maelewano kuhusu Azimio la Bunge na kwamba muafaka ulifikiwa Azimio hili lisitekelezwe, yaani Serikali ya Tanganyika isiundwe.
“Mwaka 1994, Halmashauri Kuu ya CCM ilipitisha azimio kuhusu haja ya kuendelea na muundo wa serikali mbili kwa lengo la kufikia muundo wa serikali moja,” alisema.
Alisema baada ya Tume ya Jaji Nyalali, serikali iliunda Kamati ya Shellukindo ikijumuisha wajumbe kutoka serikali zote mbili na Serikali ya Zanzibar nayo ikiunda Kamati ya Amina Salum Ali.
“Kamati ya Shellukindo ilichambua mambo yote ya Muungano na kutoa mapendekezo ya kuboresha utekelezaji. Lakini pia ilitoa mapendekezo ya baadhi ya mambo kuondolewa kwenye Orodha ya Mambo ya Muungano, kwa mfano, bandari.
“Kwa upande mwingine Kamati ya Amina, pamoja na mambo mengine, ilipendekeza mambo 12 yaondolewe kwenye Orodha ya Mambo ya Muungano. Mambo hayo yalihusu uchumi.
Mwaka 1994, serikali zote mbili zilikutana kutafakari mapendekezo ya Kamati ya Shellukindo.
“Pamoja na mambo mengine muafaka ulifikiwa kuondoa au kubadili baadhi ya mambo kwenye Orodha ya Mambo ya Muungano,” alisema Warioba.
Alisema kwa kuwa mjadala juu ya Muundo wa Muungano ulikuwa unaendelea wakati wote, serikali ikaona ni busara kuunda Kamati ya Jaji Kisanga ambayo, pamoja na mambo mengine, ilitakiwa kupendekeza aina ya muundo wa Muungano na Kamati ya Kisanga ilipendekeza muundo wa serikali tatu.
“Pendekezo hili halikukubalika lakini muafaka wa 1994, kati ya serikali zote mbili, uliendelea kutekelezwa bila ya kufanya mabadiliko kwenye Katiba,” alisema

“Pendekezo hili halikukubalika lakini muafaka wa 1994, kati ya serikali zote mbili, uliendelea kutekelezwa bila ya kufanya mabadiliko kwenye Katiba,” alisema - See more at: http://raiamwema.co.tz
Post a Comment