Mwanasiasa mwenye historia ya
kipekee nchini, James Mapalala amesema ufafanuzi wa Rasimu ya Katiba
uliotolewa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba, umekiacha Chama Cha
Mapinduzi (CCM) kwenye wakati mgumu.
Mapalala,
ambaye ni mmoja wa wajumbe wa Bunge la Katiba, amesema ufafanuzi huo ni
wa kisayansi kwa kiwango cha juu kiasi kwamba atakayetaka kubishana
naye, atakabiliwa na kazi pevu ya kujenga hoja.
“Ripoti yake (ya mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba) imekuwa very scientific (ya
kisayansi sana). Kila kitu alichoeleza amekitolea ushahidi ulio hai
katika maisha ya kila siku ya Watanzania,” alieleza Mapalala.
Mapalala
alisema pamoja na kuwa una manufaa kwa mustakabali wa taifa, ufafanuzi
huo umeiweka pabaya CCM kutokana na kujibu hoja zote ambazo chama hicho
kilipanga kuzitumia kuipinga hotuba hiyo.
“Labda
watumie nguvu kubwa lakini kwa mtindo wa kutumia hoja, hakuna Mtanzania
mwenye akili timamu atakayeshindwa kubaini hali halisi inayolikabili
taifa, kwa sababu ukweli umewekwa peupe,” alieleza Mapalala.
JK akoleza mjadala
Kauli hiyo ya Mapalala
imekuja wakati tayari Rais Jakaya Kikwete amelihutubia Bunge na kueleza
kwamba inavyoonekana Muundo wa serikali tatu hautekelezeki.
Mbali na kupinga muundo wa serikali tatu na
kupendekeza serikali mbili, Rais Kikwete ameonyesha shaka kuhusu
utekelezaji wa ukomo wa ubunge uliopendekezwa na Tume ya Katiba.
Mapalala
alisema madai yanayotolewa na baadhi ya wanaotaka serikali tatu kwamba
sehemu kubwa ya maoni yaliyo katika rasimu iliyowasilishwa ni maoni
binafsi ya Jaji Warioba, yanakosa mashiko kwa sababu sasa kila “mwenye
macho haambiwi tazama.”
Anasema hata madai kwamba mahitaji ya serikali tatu ni ya kisiasa; ikielezwa kuwa CUF inaamini itatawalaZanzibar kadhalika Chadema ikijiamini kuwa kitatawala Tanzania Bara, hayana msingi.
Alisema
haoni mantiki ya CCM kumpinga Jaji Warioba kwa kuwa Tume ya Mabadiliko
ya Katiba imeundwa na Serikali ya chama hicho tawala chini ya mwenyekiti
wake, Rais Jakaya Kikwete.
“Hata
marekebisho ya sheria hiyo, yaliyofanyika Septemba mwaka jana
yalipitishwa huku vyama vya upinzani vyenye uwakilishi bungeni vikiwa
havipo ndani ya vikao; ikaidhinishwa kuwa tume ikimaliza kuwasilisha
rasimu uhai wake uwe umekoma. Ikiwa kwenye mchakato huu kuna siasa, basi
zinaletwa na CCM na si vinginevyo,” alieleza Mapalala.chanzo............
Post a Comment