
Unapoingia katika nyumba ya familia ya Salehe Saidi, macho na masikio yako hayawezi kukwepa ucheshi wa kijana wa miaka 13, Jumbe Salehe. Ni kijana anayeipa tabasamu familia hiyo.
Jumbe ni mwenye nguvu, afya, akili darasani na uchangamfu ambao kila mzazi angependa kuuona kwa kijana wake. Lakini Jumbe Salehe, hakuzaliwa kama watoto wengine. Alipatikanaji katika mchakato mrefu, uliohusisha teknolojia ya hali ya juu na majaribio yaliyohitaji werevu. Jumbe alizaliwa kwa njia ya upandikizaji wa mbegu ambao kwa jina la kitaalamu unajulikana kama In-Vitro Fertilization (IVF). Mchakato huo ulisimamiwa na Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Wanawake, Profesa Malise Kaisi.
Kwa nini Jumbe alizaliwa kwa njia ya IVF?
Mwanaidi Kombo, mama mzazi wa Jumbe, hakuwa na tatizo la uzazi hapo awali. Alifanikiwa kupata mtoto wake wa kwanza mwaka 1986.
Mwaka 1988 alipata ujauzito mwingine lakini kwa bahati mbaya, uliharibika na kuanzia hapo ikawa ni vigumu kwake kushika mimba nyingine.
“Baada ya kuhangaika kwa muda mrefu nikajaribu kupata mtoto, lakini tatizo jingine likaanza. Mwaka 1990. Nilianza kupata maumivu makali ya tumbo,” anasema Mwanaidi.
Kutokana na maumivu hayo, alianza kusaka msaada wa kitabibu na alishauriwa kwenda kwa daktari wa magonjwa ya wanawake, Dk. Malikiti wa Hospitali ya MM.
Safari yake kwenda kwa daktari ilimsaidia kung’amua ukweli, kwani aliambiwa kuwa ana uvimbe mkubwa kwenye kizazi ambao unaweza kuhatarisha maisha yake na kuwa ndicho chanzo cha kushindwa kupata mtoto.
Hata hivyo, Dk. Malikiti alimuelekeza aende kuonana na Profesa Kaisi kwa kuwa ndiye mtaalamu wa masuala ya uzazi kwa wanawake.
“Nilipofika kwa Dk. Kaisi, nilimshangaa baada ya kuisoma picha ya Xray. Aliniambia niache kabisa kunywa dawa nilizoandikiwa za maumivu na kuambia ninywe panadol endapo nitakuwa na maumivu,” anasema.
Ingawa Mwanaidi alishangaa, aliendelea na kliniki ya Dk. Kaisi akihudhuria kila wiki kwa zaidi ya miezi miwili. Siku moja Dk. Kaisi akaamua kumfanyia kipimo cha CT Scan kuangalia mirija ya uzazi na ndipo alibaini kuwa pamoja na uvimbe, mrija wake mmoja umepinda Endea na story
Post a Comment