MAMBO MAKUBWA MATANO (5) YANAYOKOSEKANA KATIKA RASIMU YA KATIBA









1 Haki ya Msingi kwa ajili ya Ustawi wa Watu.

· Haki ya Afya

· Haki Ya Hifadhi ya jamii

· Ulinzi wa kutosha kwa haki ya kuishi

· Haki ya Msaada wa sharia

2 Bado kuna ombwe katika msingi upatikanaji wa baadhi ya watumishi wa umma

a. Bado wajumbe wa Tume ya Utumishi wanateuliwa na rais –ibara ya 73(2)

b. Utaratibu wa kuthibitisha watumishi kupitia bunge hauna uhakika wa kuondoa dosari za uteuzi kwa asilimia mia moja-ibara ya 98(1),99(1),104(1),105(1)

3 Taasisi za uwajibikaji hazijapewa mamlaka ya kutosha

a. Tume ya haki za binadamu haitakuwa na uhuru ikiwa fedha zake hazitatoka mfuko mkuu wa fedha za serikali-ibara ya 207

b. Rasimu haijatambua taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa kama taasisi za kikatiba

c. Madaraka ya taasisi hizi kuwajibisha viongozi mbalimbali wa kitaifa hayajawekwa wazi

4 Muundo wa Muungano unahitaji kuboreshwa zaidi

a. Rasimu haijaweza kubainisha tofauti kati ya dola nan chi – ibara ya 1

b. Haki za binadamu zinapaswa kuwa moja ya mabo muhimu ya muungano-ibara ya 63 na nyongeza katika katiba

c. Masuala ya mahusiano ya kitaifa na mabo ya nje yanafaa kubaki katika mamlaka ya jamhuri ya muungano –ibara ya 65(2)

d. Madara ya marais/viongozi wan chi wa shirika dhidi ya rais wa jamhuri ya muubgano yanapaswa yawekwe bayana –ibara ya 69

e. Makao makuu ya jamhuri ya muungano hayajatajwa katika rasimu.

5 Kunahitajika ufafanuzi kuhusu mfumo wa uchumi, rasilimali na mgawanyo wa pato la taifa kwa wananchi

a. Suala la rasilimali ardhi kama mali ya wananchi wa Tanzania halijapewa umuhimu

b.Rasilimali nyingine kama gesi, madini na mafuta hazijafafanuliwa jinsi zitakavyonufaisha jamhuri ya Mmuungano.

c.Rasimu haijaweka bayana aina ya mfumo wauchumi ikiwa ni ujamaa au ni ubepari ambao taifa litaufuata. chanzo www.humanrights.or.tz

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright WORLD OF TODAY Published.. Blogger Templates
Back To Top