MAMBO YA MSINGI ALIYO YASEMA JAJI WARIOBA



Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba amesisitiza kuwa mapendekezo ya serikali tatu katika Muungano ni ya wananchi na taasisi mbalimbali, na wala si matakwa ya tume yake.


Akiwasilisha Rasimu ya Pili ya Katiba wakati wa kikao mahsusi cha Bunge Maalum mjini Dodoma, Jaji Warioba alieleza kuwa nusu ya wananchi waliotoa maoni yao kuhusu Muungano walitaka uwepo wa serikali tatu.


Kati ya wananchi 38,000 waliotoa maoni yao kuhusu Muungano, 19,000 walizungumzia suala la muundo, huku zaidi ya nusu wakitaka marekebisho ya kikatiba yatakayowezesha uwepo wa serikali tatu.

“Kwa upande wa Bara, asilimia 61 [ya wale waliotoa maoni juu ya Muungano] walipendekeza muundo wa serikali tatu,” alisema Jaji Warioba. “Kwa upande wa Zanzibar, [asilimia] 60 walipendekeza Muungano wa mkataba.” Clink hapa kuangalia video

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright WORLD OF TODAY Published.. Blogger Templates
Back To Top