Mwanahabari ‘aliyeua’ Wanahabari bungeni

 



Dk Harrison Mwakyembe, mwandishi wa habari kitaaluma aliyeingia katika historia ya aina yake, kwa kushiriki kuunga mkono hoja ya kuzuia wanahabari wenzake kuingia na kuandika habari ndani ya Kamati za Bunge Maalumu la Katiba.


Maswali mengi kuliko majibu yameibuliwa na uamuzi wa Dk. Mwakyembe, kusimama upande mmoja na wanaodhani siyo sawa kwa wanahabari kupata na kuwafahamisha wananchi juu ya mchakato wa kutunga Katiba, unavyofanyika hatua kwa hatua, kuanzia kwenye Kamati mpaka mijadala ya wazi bungeni.


Maswali na hisia hizi zinachochewa na ukweli kwamba Dk. Mwakyembe ni Mwandishi wa Habari Kitaaluma. Kwa maneno mengine, wanahabari walimtarajia ajenge hoja ya kuwapo uhuru wa habari ndani ya kamati hizo.


Mchakato wa kukusanya maoni ulikuwa wa wazi, waandishi waliruhusiwa kwenye mabaraza ya katiba ya kata na kupakutokea madai ya kuwapo upotoshaji.


Ndani ya mabaraza hayo, ambaye hakuwa Mjumbe wa Baraza la Katiba hakuruhusiwa kuingia, isipokuwa watumishi wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba na waandishi wa habari; huko nako kifungu kimoja baada ya kingine cha Rasimu ya Kwanza ya Katiba, kilijadiliwa.


Dk Mwakyembe ni nani katika tasnia ya habari


Ni mwenye Shahada ya juu (PhD) katika sheria aliyoipata kati ya mwaka 1992 na 1995, Chuo Kikuu cha Hamburg (FRG). Kabla ya hapo alikuwa na shahada ya pili kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.


Historia yake inaonyesha Dk. Mwakyembe alisomea taaluma ya uandishi wa habari katika Shule ya Waandishi wa Habari Tanzania (TSJ), kati ya mwaka 1975 na 1977 na kutunukiwa Stashahada. Dk. Mwakyembe amewahi kutumikia umma wa Watanzania kupitia taaluma hiyo, katika Shirika la Habari Tanzania (Shihata) kati ya mwaka 1978 na 1980 kabla ya mwaka 1977 alipofanya kazi Idara ya Habari (Maelezo).


Kwa hiyo Dk. Mwakyembe anafahamu vilivyo, madhila ya wanahabari hususan wale wanaofanya kazi nchini, anafahamu umuhimu wa habari kwa umma na haki ya mwananchi kupatiwa habari kwamba ni ya kikatiba.


Leo hii Dk. Mwakyembe ni mmoja wa Wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba, ambaye Machi 6, 2014 wakati wakipitia kanuni alikuwa miongoni mwa waliochangia hoja yenye kuhusu wanahabari na utendaji wao kwenye Bunge hilo.


Hivi ndivyo Daktari huyu alivyo‘ua’ wanahabari wenzake Bungeni, endelea kufuatilia maneno yake:


Mheshimiwa Mwenyekiti hii ni mara yangu ya kwanza kusimama kwenye semina yako hii. Nawaomba waheshimiwa wabunge wenzangu, tusiendelee na mvutano huu, kazi iliyo mbele yetu ni kubwa na wananchi wanatuangalia. endelea..............

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright WORLD OF TODAY Published.. Blogger Templates
Back To Top