Nassari aumbuka bungeni…. Soma kwa habari kamili


Mjumbe wa Bunge Maalumu la Katiba, Joshua Nassari, juzi
alijikuta akiumbuka bungeni baada ya kushindwa kutaja kanuni
aliyoitumia, kuomba mwongozo.


Hali hiyo ilitokea muda mfupi kabla ya wajumbe kupiga kura za kumchagua Mwenyekiti wa Bunge hilo.


Kuumbuka kwa mjumbe huyo ambaye pia ni Mbunge wa
Arumeru Mshariki, kulitokana na Mwenyekiti wa Muda wa Bunge hilo, Pandu
Ameir Kificho, kumtaka kutaja kanuni aliyoitumia.




Hata hivyo, baada ya kusita kwa muda Nassari bila
kutaja kanuni aliyoitumia, alisema wajumbe wengi hawajasikia utaratibu
unaotumika katika upigaji kura kwa sababu walichelewa kwenye msongamano
wa watu getini.


“Wengi wetu tumeingia tukiwa tumechelewa kwa
sababu wengi tunapita katika geti moja. Ningependa ufafanuzi wako kuhusu
aina ya kura tunayokwenda kupiga ni ya wazi au ya siri,”alisema.


Hata hivyo, kificho alimjibu kuwa kura zitakazopigwa kumchagua mwenyekiti zitakuwa ni za siri. Hatua hiyo imekuja muda mfupi baada ya Bunge hilo
kupitisha kanuni za uendeshaji wake ambapo hata hivyo nyingine bado
zimekuwa na mgongano wa maridhiano kwa baadhi ya wajumbe kutaka
ufafanuzi zaidi

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright WORLD OF TODAY Published.. Blogger Templates
Back To Top