TANGAZO KWA WALIMU WAPYA 2013/2014

          TANGAZO                               TANGAZO                      TANGAZO

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
OFISI YA WAZIRI MKUU ‐ TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA
AJIRA MPYA YA WALIMU WAPYA KWA AJILI YA SHULE ZA MSINGI, SEKONDARI NA VYUO VYA
WALIMU ‐ MWAKA 2013/14
A: ORODHA YA WALIMU NA VITUO VYA KAZI
Ofisi ya Waziri Mkuu ‐ TAMISEMI Inatangaza Orodha ya Vituo vya Kazi kwa Wanachuo
wahitimu wa Mafunzo ya Ualimu kama ifuatavyo:‐
1. Walimu wa Cheti (Daraja IIIA) kwa ajili ya shule za msingi 17,928
2. Walimu wa Stashahada kwa ajili ya shule za sekondari 5,416
3. Walimu wa Shahada kwa ajili ya shule za sekondari 12,677
B: MATAKWA YA KILA MWALIMU
Kila Mwalimu ( Ajira Mpya) atatakiwa kuzingatia yafuatayo:‐
1. Kuripoti tarehe 01/04/2014 kwenye ofisi za Wakurugenzi wa Halmashauri kwa ajili ya
kupangiwa vituo vya kazi na kuanza kazi.
2. Mwalimu atatakiwa kuwa na vyeti vyake halisi vya Chuo na Sekondari.
3. Walimu ambao ni waajiriwa wa Serikali waliokuwa wanajiendeleza kielimu wanatakiwa
kurudi kwa waajiri wao ili kuendelea na kazi.
4. Fedha za kujikimu za siku saba (7) na nauli kwa walimu wapya zimetumwa katika
Halmashauri walikopangwa. Hivyo, kila mmoja aripoti katika Halmashauri aliyopangwa.
5. Mwalimu ambaye hataripoti ifikapo tarehe 10/04/2014 hatapokelewa tena na atakuwa
amepoteza ajira yake.
NB:
Walimu hawa wamepangwa katika Halmashauri na shule za mazoezi za vyuo vya ualimu
Tanzania Bara.CHANZOhttp://www.pmoralg.go.tz/menu-data/adverts/ajira/

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright WORLD OF TODAY Published.. Blogger Templates
Back To Top