Warioba afunguka,atoa ufafanuzi wa baadhi ya hoja za taarifa yake



Afafanua utata ulioibuliwa katika taarifa yake mbele ya Bunge la Katiba.


Dar es Salaam. Wakati Ikulu ikitangaza kwamba Rais Jakaya Kikwete amevunja Tume ya Mabadiliko ya Katiba, tume hiyo imetoa ufafanuzi wa baadhi ya maeneo ya Rasimu ya Katiba.


Taarifa ya Ikulu iliyotolewa jana, ilieleza kuwa Tume ya Jaji Joseph Warioba ilivunjwa tangu Machi 19, ikiwa ni siku moja baada ya kuwasilisha Rasimu ya Katiba bungeni mjini Dodoma.


Wakati taarifa ya Tume ya Warioba ilitolewa jana jioni, Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu ilikuwa imeshatoa taarifa ya kuvunja tume hiyo mapema jana ikieleza kuwa shughuli za tume hiyo zilikoma tangu Jumatano iliyopita.


“Kwa mujibu wa kifungu cha 31 cha Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, Rais wa Jamhuri ya Muungano alivunja rasmi Tume ya Mabadiliko ya Katiba tarehe 19 Machi, 2014 kwa Tangazo la Serikali Na.81 la tarehe 21 Machi, 2014,” ilisema taarifa hiyo ya Ikulu.


Hata hivyo, Jaji Warioba aliliambia gazeti hili jana kuwa hadi wanakutana juzi kwenye kikao cha mwisho cha tathmini walikuwa hawajapokea barua ya kuvunjwa kwa tume yake.


“Barua ya Ikulu tumeipokea leo. Tulikuwa hatuna taarifa kwamba tume yetu imevunjwa hadi tulipopokea barua leo (jana). Tulifanya kikao chetu cha mwisho cha tathmini jana (juzi),” alisema Warioba alipozungumza na Mwananchi jana jioni.


Warioba pia alithibitisha kwamba taarifa ya ufafanuzi (imechapishwa ukurasa wa 37) ni ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba.


Taarifa hiyo ya Tume ya Warioba imetaja baadhi ya sababu za kupendekezwa kwa muundo wa serikali tatu kuwa, ni pamoja na Serikali ya Muungano kutokuwa tena na nguvu upande wa Zanzibar na Rais kupokwa baadhi ya madaraka aliyopewa kikatiba.


Ufafanuzi wa Tume


Taarifa hiyo ya tume ilisema: “Waasisi walituachia mambo 21 (ukiacha usajili wa vyama) kwenye orodha ya Muungano. Katika kipindi cha miaka ishirini iliyopita yamepunguzwa. Mambo yote yaliwekwa kwa utaratibu uliowekwa na Katiba lakini yameondolewa kinyume na Katiba.” Iliongeza: “Sehemu zote mbili ziliamua kuachia baadhi ya mambo yake kuwa chini ya Serikali ya Muungano, sasa sehemu moja inaondoa mambo yake. Kwa hiyo Serikali ya Muungano itakuwa inashughulikia zaidi mambo ya upande mmoja.endelea...........

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright WORLD OF TODAY Published.. Blogger Templates
Back To Top