Changamoto lukuki zaiweka Tanzania njiapanda







Leo ni Siku ya Malaria Duniani. Ni kumbukumbu inayofanyika wakati ugonjwa huo kwa miaka mingi unaliumiza kichwa kwa sehemu kubwa Bara la Afrika hasa Kusini mwa Jangwa la Sahara.


Ugonjwa huo umesababisha vifo, ulemavu, umechochea umaskini na pia ni chanzo cha taifa kutumia kiasi kikubwa cha fedha zake kwa ajili ya kupambana na maradhi hayo.


Licha ya hatua kubwa kupigwa katika mapambano dhidi ya malaria, zipo changamoto nyingi ambazo ama zimerudisha nyuma juhudi za wataalamu wa afya baadhi yake zikiwa ni wanadamu kuchangia katika usambazaji wa vimelea vya malaria.


Takwimu za Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO) zinaonyesha kuwa kesi milioni 207 ya watu wanaogua malaria yalionekana mwaka 2012 huku kukiwa na vifo 627,000 vilivyosababishwa na maradhi hayo.


Inaelezwa kuwa wapo watu wanaoonekana au kujisikia wazima bila dalili yeyote ya malaria, lakini wanatembea na ugonjwa huo na pindi mbu wanapowauma, huchukua vimelea vya ugonjwa huo kutoka katika damu zao na kuvisambaza kwa watu wengine.


Mtafiti mwandamizi wa Taasisi ya Malaria Ifakara, Dk Seif Shekalage anasema kiwango kinachosababisha malaria hutegemea mtu na mtu. Wapo watu ambao wakiugua malaria huumwa hata kama wana kiwango kidogo cha wadudu, lakini wengine wasiumwe.


“Kuna watu wana kinga kubwa ya mwili hata kama wana vimelea vya malaria kwenye damu, basi wanaweza wasiugue kwa sababu kinga inapambana na vimelea lakini wale wenye kinga ndogo hasa kundi la wanawake wajawazito na watoto, huugua kwa urahisi pindi wanapopata maambukizi,” anasema Dk Shekalage.


Kwa mujibu wa Dk Shekalage, mbu anapomuuma mtu ambaye ana malaria lakini hajapata tiba, basi mbu huyo huchukua vimelea hivyo na kuvisambaza pale anapomng’ata mtu mwingine.


“Hii ni changamoto kubwa katika vita vya kupambana na malaria kwa sababu husababisha kusambazwa kwa maradhi haya licha ya jitihada,” anasema.


Wakati tukiadhimisha Siku ya malaria Duniani, Dk Shekalage pia anazitaja changamoto nyingine zinazorudisha nyuma vita dhidi ya malaria na kusema kuwa ni usugu wa dawa.


Anasema dawa nyingi za kutibu malaria zimekuwa sugu na kusababisha vimelea kutokufa na hivyo maradhi kumrudia mgonjwa.


“Si hivyo tu, hata viatilifu navyo vimekuwa dhaifu, kwa mfano dawa zinazowekwa kwenye chandarua nazo zimekuwa dhaifu kwa sababu mbu wamekuwa sugu, dawa za mbu nazo zimekuwa dhaifu, hivyo kusababisha wadudu kupata usugu,” anasema na kuongeza:

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright WORLD OF TODAY Published.. Blogger Templates
Back To Top