Shibuda, Arfi: Tupo tayari kuadhibiwa Chadema,



Dar es Salaam: Wabunge wa Chadema, Said Arfi na John Shibuda wamesema hawana hofu yoyote juu ya uamuzi utakaochukuliwa dhidi yao na uongozi wa chama hicho kwa kitendo chao cha kuhudhuria vikao vya Bunge Maalumu la Katiba.


Wakati Shibuda na Arfi wakieleza hayo, Mbunge wa Viti Maalumu wa chama hicho, Leticia Nyerere ameibuka na kudai kuwa hakuwahi kushiriki katika vikao vya Bunge hilo, ila alipita tu Dodoma akielekea Kwimba, Mwanza.


Kwa nyakati tofauti wabunge hao ambao kurejea kwao bungeni ni tofauti ni msimamo wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) wa kutoshiriki vikao vya Bunge la Katiba, wamesema Chadema hakina demokrasia ya kweli kama kinavyojipambanua kwa wananchi.


Mwanasheria mkuu wa Chadema, Tundu Lissu kwa nyakati tofauti amekaririwa akisema kuwa wabunge wote wa chama hicho wanaokiuka msimamo wa Ukawa kwa kuingia katika Bunge la Katiba, wajiandae kuongeza idadi ya ‘wabunge wa mahakama’.


Shibuda (Maswa Mashariki) alisema hana wasiwasi wowote juu ya uamuzi utakaochukuliwa na chama chake, kusisitiza kuwa iwapo atatimuliwa ndiyo atajua nini cha kufanya.


“Huwezi kuzungumzia kutibu kidonda wakati hujapata jeraha. Ukishapata jeraha ndiyo utajua ulitibu vipi, ushonwe nyuzi au uweke bandeji,” alisema Shibuda.


Shibuda ambaye ameshikilia msimamo wake wa kuhudhuria vikao vya Bunge la Katiba kwa ajili ya kutetea masilahi ya wakulima wa pamba na wafugaji, alisema uamuzi wa yeye kutafuta chama kingine umetoka kwa wananchi wa jimbo lake.


“Wabunge wa Chadema walisusia vikao vya Bunge la Katiba kukwepa matusi, sasa iweje leo wao wageuke vinara wa kuwatusi wenzao. Kwa muda mrefu nimeitwa msaliti na pandikizi la CCM. Nimetukanwa sana sasa nimechoka,” alisema Shibuda na kuongeza:


“Ukawa lazima wajidhihirishe kuwa wao ni kimbilio la wananchi na si kutaka madaraka tu. Siwezi kuacha kuwawakilisha wananchi wa Maswa kwa sababu ya Ukawa, hivi hao Ukawa wataleta mbegu bora ya pamba kwa wananchi?”


Alisema mbunge akiwa bungeni hata kama itapatikana Katiba ambayo haijatokana na maoni ya wananchi, sauti yake juu ya jambo alilokuwa analitetea itasikika na hatahukumiwa kwa jambo lolote.


Akizungumza katika kipindi cha Jambo Tanzania kinachorushwa na Televisheni ya Taifa (TBC1), Arfi (Mpanda Mjini) alisema: “Sihofii kabisa ila nina hofu ya Mungu tu. “Nashangaa wakati tunaanza harakati za kukijenga chama, tulikuwa tunawabeza CCM kwa kuendeshwa kibabe na kauli za ‘zidumu fikra za mwenyekiti’, lakini nashangaa sisi (Chadema) ndiyo tumeanza kuonyesha dalili za kutumikia kauli hizi.” Akifafanua sababu za kurejea katika Bunge hilo, Arfi alisema yeye ni mbunge wa wananchi na wamemtuma kuwakilisha kero na changamoto zinazowatesa kwa miaka mingi endelea kwa kubofya hapa

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright WORLD OF TODAY Published.. Blogger Templates
Back To Top