MBUNGE wa Arumeru Mashariki, Joshua Nassari (CHADEMA) jana alifikishwa Mahakama ya Mwanzo Maji ya Chai na kusomewa shtaka la uharibifu wa mali na kuchoma bendera ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), yenye thamani ya Sh laki mbili na elfu tano.
Mbunge huyo alisomewa shtaka hilo mbele ya Hakimu, David Mwita.
Ilidaiwa na upande wa mashitaka kuwa juzi saa 11:00 jioni Mbunge huyo alichoma bendera za CCM kwa makusudi zenye thamani ya Sh 205,000 huku akijua kuchoma bendera hiyo ni ukiukwaji wa kanuni na sheria za nchi.
Hata hivyo, Nassari alikana kuchoma bendera hiyo na kupewa dhamana, ambapo wadhamini watatu walijitokeza na kusaini bondi ya Sh milioni 1.5.
Mbunge huyo anatetewa na mawakili watatu, ambao ni James Millya, Charles Adiel na Marceline Bandiye. Kesi hiyo imeahirishwa hadi Desemba 24, mwaka huu.habari leo
Post a Comment