
Mwanzoni kompyuta mpakato hazikuwavutia watu wengi kwa sababu ya
kuuzwa kwa bei kubwa. Pia umbile lake kubwa halikuwapendezwa watumiaji
wengi.
Hata hivyo, hivi sasa kompyuta za aina hiyo
zimebadilshwa na kuwa na maumbo tofauti tofauti lakini zikitofautiana
bei. Ni uwezo wako wa ‘mfuko’ kwani kuna aina nyingi za kompyuta hizi na
nyingine zikiwa na gharama nafuu.
Kwa Tanzania kompyuta mpakato zinazonunuliwa kwa
kiwango kikubwa ni pamoja na Dell , ASUS , Lenovo, IBM, HP, Samsung,
APPLE , Acer, CHILLBLAST, ALIENWARE, Toshiba, SCHENKER, MSI, GIGABYTE,
Sony na SCAN.
Ununuzi msimu wa sikukuu
Msimu wa sikukuu za mwisho wa mwaka umewadia, kuna
matangazo mengi ya bidhaa mbalimbali zikiwamo kompyuta mpakato. Makala
hii inatoa mwongozo wa kuchagua bidhaa bora kuelekea mwisho wa mwaka
2014.
Ukienda kwenye maduka utakuta kuna laptop aina
tatu; zile zenye mifumo endeshi hasa windows; zisizo na mfumo endeshi na
zile zenye mifumo ya majaribio ambazo mtu atapaswa kuingia katika
mtandao maalumu kununua.
Bei za laptop zinategemea moja ya mambo hayo
matatu muhimu na zile zisizokuwa na window aghalabu bei yake ni ndogo na
inawezekana ukanununua kwa chini ya dola za Marekani 200.
Hivi sasa window 10 inafanyiwa marejeo, unaweza
kuingia dukani ukaambiwa ndio toleo jipya ukakubali kuitumia, kumbe ni
imewekwa kwa muda tu kwani baada ya muda itakusumbua. Unashauriwa utumie
windows 7 au 8.
Kabla ya kuamua kununua laptop hakikisha unajua
kile unachotaka kufanya katika laptop husika. Kwa mfano, kama ni kwa
masuala binafsi tu madogo au ya kitaaluma.
Mathalan, kama unataka kununua ya kuchezea michezo, unatakiwa kuchagua yenye viwango na uwezo mkubwa wa CPU na RAM.
Kama ni kwa ajili ya kuandika vitu vyako tu,
kutembelea tovuti mbalimbali unaweza kununua laptop ya viwango vidogo na
utatumia gharama ndogo kifedha.
CPU ndiyo mwendeshaji mkubwa wa laptop yako, udogo
au ukubwa wa CPU ndiyo unaoamua kasi ya laptop yako kutokana na
matumizi. Kuna kampuni nyingi zinazotengeneza CPU Kama Intel, AMD,
Motorola na nyingine Mwananchi
Post a Comment