Taarifa ya Ndege iliyopotea



Shughuli ya kutafuta ndege ya AirAsia ambayo ilipotea jana Jumapili imeendelea leo tena baada ya zoezi hilo kusitishwa kwa muda.


Ndege za kijeshi kutoka indonesia na singapore zilikuwa zikiisaka ndege hiyo kusini magharibi mwa pwani ya Borneo ambapo ndege hiyo ilitoweka.


Ndege ya AirAsia ya Indonesia imepotea usiku wa kuamkia jana ikiwa na abiria 162 ikitokea Surabaya nchini humo kwenda Singapore.


Habari za kupotea ndege hiyo QZ8501 zilianza kutolewa katika akaunti mbalimbali za Twitter za vyombo vya habari vya kimataifa saa 12.30 asubuhi kwa saa za Afrika Mashariki na kufuatiwa na taarifa ya Kampuni ya AirAsia Indonesia iliyotolewa kupitia akaunti yake ya Facebook.


Tukio la kupotea kwa ndege ni la pili mwaka huu baada ya ndege ya Shirika la Ndege la Malaysia, MH370 iliyokuwa ikitokea Kuala Lumpur, Malaysia kwenda Beijing – China, kupotea Machi ikiwa na abiria 239 na hadi sasa haijapatikana.


Ndege nyingine ya Malaysia, MH17, ilitunguliwa kwa kombora huko Ukraine Julai 17 na kusababisha vifo vya abiria wote 298 waliokuwamo.


Taarifa ya AirAsia Indonesia


Taarifa zilizopatikana kutoka vyanzo mbalimbali vya kimataifa zilisema marubani waliomba kuichepusha njia kadri ya maelekezo ya waongozaji wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga ya Indonesia (CAA) kutokana na hali mbaya ya hewa lakini baadaye ikapoteza mawasiliano.


Uongozi wa kampuni hiyo ulibainisha kuwa ndege hiyo aina ya Airbus 320-200 yenye namba za usajili PK-AXC, iliondoka kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Juanda, Surabaya saa 11.35 (Tanzania saa 7.35 usiku) na kupoteza mawasiliano na waongozaji wake saa 1.24 asubuhi (9.24 usiku).


“Ndani ya ndege kulikuwa na abiria 155 ambao kati yao watu wazima ni 138, watoto 16 na mto mchanga mmoja. Pia, walikuwamo marubani wawili, wahudumu wanne na mhandisi wa ndege mmoja,” ilieleza sehemu ya taarifa hiyo na kuongeza kuwa kati yao, 156 ni Waindonesia, Wakorea Kusini watatu na raia mmoja mmoja kutoka Ufaransa, Malaysia na Singapore.


Kwa mujibu wa AirAsia, mara ya mwisho ndege hiyo ilifanyiwa matengenezo ya kawaida Novemba 16. Hata hivyo, habari zaidi kutoka tovuti ya airfleets.net zilionyesha kuwa ndege hiyo ilikuwa matengenezoni kwa kipindi cha zaidi ya miaka sita. Shirika la habari la Uingereza (Reuters), lilimkariri Mkurugenzi wa Uchukuzi wa Wizara ya Uchukuzi wa Anga wa Indonesia, Joko Muryo Atmodjo akisema hadi jana mchana hakukuwa na mawasiliano yoyote tena na ndege hiyo mwananchi

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright WORLD OF TODAY Published.. Blogger Templates
Back To Top