MKUTANO WA KIHISTORIA MTWARA MJINI
NI VIWANJA VYA MASHUJAA MTWARA MJINI 31/12/2014 SAA NANE MCHANA.
Professa Ibrahim Lipumba bingwa wa uchumi duniani ambaye pia ni mwenyekiti mwenza wa ukawa KUUNGURUMA pamoja na
Zitto Zuberi Kabwe Mwami Luyaga(MB) ambaye pia ni mwenyekiti wa kamati ya PAC KUZUNGUMZA pamoja na
Wabunge watano wa JMT wanaotokana na Umoja wa katiba ya wananchi UKAWA WATAONGEA siku hiyo.
Kivutio kikubwa siku hiyo ni ZITTO KABWE akiwa pamoja na mchumi NGULI wa dunia Profesa LIPUMBA katika jukwaa moja.
Safari ya UKOMBOZI ina anzia MTWARA sehemu muhimu katika uchumi wa kisasa kutokana na upatikanaji wa GESI na MAFUTA.
ZITTO aliyejizolea umaarufu wa kufanya tafiti za kisomi ana Shahada ya uzamili ya sheria na biashara ni MSOMI kijana.
Prof LIPUMBA ana Shahada ya udaktari wa falsafa (PhD) maeneo yake ya utaalamu ni(a)Maendeleo ya uchumi (b) Uchumi wa Kilimo (c)Biashara za Kimataifa na Fedha(d) Uchumi Mpana (Macroeconomics) ni M/kiti wa JOPO la Maprofesa bingwa wa uchumi duniani.
Taarifa zilizopo ZITTO KABWE na Professa LIPUMBA kuzunguka nchi nzima baada ya MTWARA.
ZITTO kufafanua wizi wa Escrow kwa kuwataja majina wezi wote na viwango vya fedha walivyochukua
Professa LIPUMBA kueleza namna TANZANIA inaweza kuondokana na umasikini kama itafuata ushauri wake.
HII NI TAREHE 31/12/2014 SAA 8:00 MCHANA VIWANJA NI MASHUJAA MTWARA MJINI .habari24 blogspot
Post a Comment