MAAJABU: Chemchemi ya moto iliyogeuzwa bafu la kijiji



Rufiji. Watu wanaosema kuwa Mungu ndiye muumbaji wa vitu vyote huamini kwamba mwanadamu anao ukomo wa kuviona na hata kuvitolea maelezo baadhi ya vitu anavyoviona.


Watu hao pia huamini kwa kuwa hawawezi kutoa tafsiri sahihi au kubainisha chimbuko la baadhi ya vitu vya asili wanavyoviona au kuvisikia, huamua kusema, ‘tunamwachia Mungu’.


Hivi karibuni nikiwa katika Kijiji cha Utete, wilayani Rufiji katika Mkoa wa Pwani, nilitembelea moja ya vivutio vinavyosifika mkoani humo na hata Tanzania nzima.


Kivutio hicho ni chemchemi ya maji ya moto ambayo hakuna anayejua ilianza lini, kwa kuwa wazee katika eneo hilo wanasema hata wakoloni waliikuta na kwamba wazungu hao ndiyo waliokuwa wa kwanza kujenga uzio katika eneo hilo.


Ukiwa unakwenda kwa mara ya kwanza katika chemchemi hiyo iliyopo mita chache kutoka Utete mjini, kichwani utakuwa na picha nyingi za kufikirika kuhusu eneo hilo, ambazo pengine hazisadifu uhalisia.


Kutoka barabara kuu inayoingia makao makuu ya wilaya, ipo njia ndogo ya kupita magari yanayoelekea mahali ilipo chemchemi hiyo.


Hatua chache kabla ya kuyafikia maji hayo, utaona kwa mbali kisima kimezungushiwa ukuta, lakini sehemu ya juu imeachwa wazi.


Unavyozidi kusogeza zaidi, utaona moshi ukitoka ndani ya kisima hicho unaoashiria kuwa maji yaliyomo ndani yanachemka.


Ukisogea karibu zaidi utagundua kuwa ukuta huo ulijengwa miaka mingi iliyopita, ingawa upande mmoja umerekebishwa hivi karibuni.


Kwa kuwa unataka kuthibitisha kama kweli maji hayo ni ya moto; utatafuta sehemu angalau uyaguse kwa ncha ya kidole, ndipo uamini kuwa macho yako yanachokiona ni sahihi.


Kwa kuwa eneo la chemchemi hiyo ni kubwa, umejengwa mfereji unaowezesha maji kutoka na kuelekea katika bwawa lililopo karibu na eneo hilo.


Bafu la kijiji mwananchi

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright WORLD OF TODAY Published.. Blogger Templates
Back To Top