Sugu anusurika kifo, apata ajali mlima Kitonga, cheki picha hapa


Mbunge wa Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi akielekeza namna ajali ilivyotokea. Picha kwa hisani ya Mbeya Yetu Blog 

Dar es Salaam. Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi (Chadema) amenusurika kifo baada ya kupata ajali katika Milima ya Kitonga, Wilaya ya Kilolo mkoani Iringa.


“Shetani amefeli, Mungu ni mwema. Tuko salama mimi na wote niliokuwa nao kwenye gari,” alisema mbunge huyo anayejulikana zaidi kwa jina la Sugu, katika ujumbe alioutuma kwenye ukurasa wake wa facebook.


Akizungumza kwa simu kutoka eneo la tukio, katibu wa Sugu, Mkwame Anangisye alisema ajali hiyo ilitokea jana saa 9:30 alasiri wakati mbunge huyo alipokuwa akitoka Mbeya kwenda Mikumi, Morogoro kushiriki mkutano wa hadhara.


Alisema gari aina ya Toyota Landcruiser lilikuwa limebeba watu wanne na kwamba hakuna mtu aliyejeruhiwa ingawa mbunge aliyekuwa akiendesha galipata michubuko mikononi.


“Wakati tunateremka Mlima Kitonga, breki zilifeli gari likagonga gema na kupinduka matairi juu,” alisema Anangisye.


Mwaka 2013 Sugu alipata ajali na gari hilo hilo alipogongana na basi la Kampuni ya Best wilayani Hanang’ mkoani Manyara wakati akienda Arusha. mwananchi

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright WORLD OF TODAY Published.. Blogger Templates
Back To Top