Huko Miembe Saba, Kibaha, Pwani baba ametiwa mbaroni na polisi akituhumiwa kuwa amekuwa akiwabaka watoto wake wawili kwa zaidi ya miaka miwili sasa.
Bhuyo alianza kuwabaka binti zake mwaka 2013 siku ambazo mkewe, ambaye na mama wa mabinti hao, akiwa hayupo; na aliendelea uhalifu huo mpaka usiku wa Machi 19, mwaka huu. .
Polisi, pamoja na watoto hao wenyewe wenye umri wa miaka 15 anayesoma darasa la saba, na e umri wa miaka 11 aliyeanza kubakwa akiwa darasa la tatu wamethibitisha kutokea kwa tukio hilo.
Kwa mujibu wa watoto hao, baba huyo alikuwa anamuita mmoja wa watoto wake chumbani kwake na kumtaka alale na mdogo wao wa kiume wakati huo akiwa na mwaka mmoja na binti akipitiwa na usingizi humvua nguo za ndani na kumwingilia huku akimtaka kukaa kimya na kuvumilia maumivu.
Mke wa mtuhumiwa huyo, ambaye amekuwa akizimia mara kwa mara kutokana na kulia baada ya kubaini yaliyowasibu mabinti zake, alisema alifahamu kuwa watoto wake wanabakwa Ijumaa iliyopita baada ya mmoja wa mabinti zake hao kumweleza kuwa baba yake alikuwa amembaka Machi 19, mwaka huu.

Mama wa mabinti wanaodaiwa kubakwa na baba yao, Rahma Mashamu, akilia kwa uchungu wakati akihojiwa na waandishi wa habari
Alisema kabla ya binti huyo kumweleza hivyo, alimwomba mama yake asimpige kwani kuna kitu anataka amweleze, japo ni kibaya lakini yeye amechoshwa na kimekuwa kikimuumiza.
“Alisema kila ninapokwenda katika biashara zangu, anatamani nisiwe ninawaacha hapo, nikamwahidi sitamfanya kitu ili mradi aseme ukweli tu,” alisema mama huyo.
Baada ya kuhakikishiwa kulindwa, ndipo binti huyo aliposimulia jinsi ambavyo baba yake amekuwa akiwafanyia na kuwatishia wakipiga kelele atawaua.
“Niliposikia mwili ulisisimka na ghafla binti yangu mwingine naye akatokea akilia na kuniambia, ‘hata mimi baba ananifanyiaga hivyohivyo kila siku unapokuwa umepeleka mboga sokoni Kariakoo,” alisema mama huyo.
Mwanamke huyo ameomba sheria ichukue nafasi yake katika tukio hilo kwa kuwa ni la kinyama na pia wataalamu wa saikolojia wamsaidie binti yake mdogo wa darasa la tano kwani yeye ameathirika zaidi.
Daktari aliyewapima watoto hao, ameshauri binti huyo mdogo apate ushauri zaidi ili kurudisha akili yake katika hali ya kawaida.
Post a Comment