Hali bado si shwari Burundi..hii inatokana na machafuko ya kisiasa yanayoendelea baada ya Rais aliyeko madarakani Pierre Nkurunziza kutaka kuwania kwa muhula wa tatu mfululizo.
Baada ya kutofikia makubaliano ikiwemo jaribio la kutaka kumpindua lililofanywa kushindikana huku watu wakiendelea kaadamana kushinikiza aondoke.
Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza amehairisha uchaguzi wa ubunge kwa siku kumi .
Msemaji wa rais Willy Nyamitwe amesema Rais huyo ameahirisha uchaguzi wa Ubunge kwa muda wa siku 10 kufuatia jaribio la mapinduzi.
Awali uchaguzi huo ulipangwa kufanyika Mei 26 na sasa utafanyika June 2 na umeahirishwa ili kupata muda wa kuwasikiliza washirika wa kimataifa pamoja na tume ya uchaguzi.
Hadi sasa tarehe rasmi ya uchaguzi wa Urais uliopangwa kufanywa Juni 26 haijabadilika
-BBC
Post a Comment