
Dodoma.
Mahakama ya Hakimu Mkazi Dodoma imeanza kuzisikiliza kesi za uhujumu uchumi,
zinazomkabili mshtakiwa Boniface Malyango maarufu ‘Shetani hana huruma’ na
wenzake wawili.
Kesi
hizo ni ya ukusanyaji, usafirishaji na uuzaji vipande 118 vya meno ya tembo
vyenye thamani ya zaidi ya Sh1.9 bilioni.
Washtakiwa
wengine ni Malyango Abdallah, Ally Chaoga maarufu Babu na Lucas Malyango
maarufu Lucas Mponze au Shimie, wote walikamatwa na maofisa wa kikosi kazi cha
Taifa cha kupambana na ujangili.
Kesi
hizo zinasikilizwa na Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Erick Fovo na
Mwajuma Lukindo.
Mawakili
wa Serikali, Paul Kadushi na Salim Msemo walidai kuwa katika kesi ya uhujumu
namba 20 ya 2015, washtakiwa hao wanakabiliwa na mashtaka mawili likiwamo la
kujihusisha na nyara za Serikali kupitia genge la uhalifu.more........
Post a Comment