Mtanzania azua tafrani katika familia ya Zuma





Dar es Salaam. Mtanzania anayeishi Afrika Kusini, Stephen Ongolo amekamatwa na polisi wa nchi hiyo akidaiwa kutishia kutoa siri za mke wa pili wa Rais Jacob Zuma, Nompumulelo Ntuli Zuma au MaNtuli.


Kwa mujibu wa magazeti ya Sunday Times na Independent ya Afrika Kusini, Ongolo alikamatwa Ijumaa, Januari 24 na alitakiwa kufikishwa katika Mahakama ya Durban juzi kabla ya kusogezwa hadi wiki ijayo.


Kabla ya kukamatwa, Ongolo aliwasiliana na magazeti mbalimbali nchini humo akidai kuwa amekuwa akilipwa, Randi 200,000 (Sh29 milioni) kwa zaidi ya miaka mitatu sasa ili afiche siri za mke huyo wa Rais.


Katika madai yake, Ongolo alisema mke wa Zuma, (MaNtuli), amekuwa akimtumia ili kupata kibali cha uchimbaji wa madini, nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).


Kwa mujibu wa magazeti hayo, kabla ya kukamatwa, Ongolo alidai kuwa anafahamu taarifa za MaNtuli kwa kina na anajipanga kuzitoa kwenye vyombo vya habari.


Alidai kuwa kuna siri kubwa ya urafiki wa MaNtuli na aliyekuwa mlinzi wake, Phinda Thomo ambaye alijiua kwa kujipiga risasi bafuni kwake, Soweto mwaka 2009.


Magazeti hayo yalimkariri Ongolo kupitia barua pepe, akisema kifo cha Thomo hakikuwa cha kujiua, bali mauaji ya kupangwa yaliyosababishwa na uhusiano wa siri kati yake na MaNtuli.


Iliwahi kuripotiwa kwamba Thomo alijiua baada ya kugundua kuwa vyombo vya habari vinachunguza uhusiano kati yake na MaNtuli.


Balozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini, Radhia Msuya alisema wamepata taarifa hizo kwa mshtuko na ofisi yake inafuatilia kujua kweli kuhusu uraia wa Ongolo.


“Ubalozi haufahamu kuhusu uraia wake. Baada ya kupata taarifa hizo tunachokifanya sasa ni kufanya uchunguzi kama kweli ni raia wa Tanzania kisha tutawaeleza,” alisema.


Msemaji wa Idara ya Uhamiaji, Naibu Kamishna, Abbas Irovya alisema watawasiliana na ubalozi kuthibitisha kama Ongolo ni Mtanzania.
Siri kuhusu Thom

soma jaidi http://www.mwananchi.co.tz/habari/Kitaifa

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright WORLD OF TODAY Published.. Blogger Templates
Back To Top