ZITTO ASHINDA MAHAKAMANI, HII HAPA HUKUMU YAKE

Zitto Kabwe ashinda hukumu ya kesi yake.....Mahakama yaizuia kamati kuu ya CHADEMA kujadili uanachama wake hadi shauri lake la msingi litakaposikilizwa

LEO macho na maskio ya watanzania hasa wafuasi na wapenzi wa CHADEMA yalielekezwa katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam,pale ambapo Jaji wa Mahakama hiyo Jaji John Utumwa alikuwa akitoa hukumu dhidi ya Zitto Kabwe na CHADEMA....


Zitto ambaye alikuwa ni Naibu Katibu Mkuu wa Chama hicho, alifungua kesi katika Mahakama hiyo akipinga hatua ya Kamati Kuu ya Chama hicho iliyokutana tarehe 3 na 4 mwezi huu kujadili hatima ya uanachama wake wakati baraza kuu halijakaa na kujadili rufaa yake...

Akisoma hukumu ya kesi hiyo baada ya kuiahirisha jana, Jaji wa mahakama hiyo,Jaji Utamwa ameridhia pingamizi lililotolewa na mh. Zitto Kabwe la kutojadili uanachama wake na kuitaka kamati kuu ya CHADEMA au chombo kingine chochote kisijadili uanachama wake hadi kesi yake ya msingi ( rufaa ) itakaposikilizwa na baraza kuu la chama hicho

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright WORLD OF TODAY Published.. Blogger Templates
Back To Top