Dk. Slaa apaniwa Mwanza











WAKATI Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Wilbroad Slaa na wabunge wengine watano wanatarajiwa kulitikisa Jiji la Mwanza, upepo unaonyesha huenda wakakumbana na wakati mgumu, kutokana na wananchi kupania kuwauliza maswali mkutanoni.

Dk. Slaa leo anatarajiwa kufanya mkutano jijini hapa, ikiwa ni mwendelezo wa Operesheni ya M4C Pamoja Daima, lakini wananchi wamekuwa katika makundi makubwa wakijadili namna ya kupata majibu ya maswali yanayowasumbua kwa muda mrefu.

Mkuu wa operesheni hiyo Kanda ya Ziwa, Tungaraza Njugu, alisema katika mkutano huo zitajadiliwa ajenda tisa na kubainisha kwamba ajenda tano za kitaifa zitazungumzwa kwa uwazi, huku ajenda nyingine zikijadiliwa kwenye vikao vya baraza la mashaurino la mkoa.

Alisema ajenda za kitaifa zitakazojadiliwa katika mkutano huo ni suala la Katiba mpya, daftari la wapiga kura, gharama za umeme, Operesheni Tokomeza Ujangili na Kimbunga pamoja deni la taifa.

Njugu alisema chama kimeona masuala hayo ni muhimu kuwaeleza Watanzania, ili waweze kujua hali halisi iliyopo ndani ya nchi yao, kwa kuwa serikali imekuwa na kigugumizi cha kuweka wazi mambo hayo.

“Dk. Slaa, ambaye leo hii (jana) yupo mkoani Mara, kesho (leo) atakuwa hapa Mwanza katika Uwanja wa Furahisha, ambao una uwezo wa kuchukua maelfu ya wananchi wa Jiji la Mwanza.

Hata hivyo, alivyotakiwa kueleza mgogoro wa Meya Matata na madiwani wake kama masuala yao yatazungumzwa kwa kuzingatia baadhi ya kata kutelekezwa kutokana na madiwani kusimamishwa zaidi ya mwaka mmoja, alisema Meya Matata hawamtambui.

Njugu alisema Meya Matata alishafukuzwa zamani na kunyang’anywa kazi, hivyo hataruhusiwa kushirika vikao vyovyote ndani ya chama hicho, kutokana usaliti wake na kuwafukuzwa madiwani watatu.

Hata hivyo, baadhi ya madiwani wa chama hicho waliliambia MTANZANIA Jumamosi kwa sharti la kutotajwa majina yao kuwa katika kikao cha Baraza la Mashauriano, wamepania kumpasha ukweli Dk. Slaa juu ya mwenendo wake.

“Unajua mwandishi hiki ni chama cha Watanzania wote, lakini jinsi kinavyoendeshwa wengine haturidhishwi, sasa lazima tumweleze Dk. Slaa ili ajue na wajirekebishe, kwani Watanzania wengi bado wana matumaini makubwa nacho,” alisema mmoja wao.

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright WORLD OF TODAY Published.. Blogger Templates
Back To Top