Hata Messi hawezi kumsaidia Wenger?






MWAKA 2001, Steven Gerrard, alikuwa akikabiliana na maswali ya waandishi wa habari siku moja kabla ya Liverpool kucheza na Arsenal katika mechi ya fainali ya Kombe la FA.


Aliulizwa kuhusu itakavyokuwa baina yake na kiungo wa Arsenal, Patrick Vieira. Jibu lake lilikuwa rahisi tu, alisema: “Vieira yuko katika daraja jingine. Nina mikanda mingi ya video inayomwonyesha Vieira akicheza uwanjani, naitumia kwa ajili ya kujifunza”.


Miaka 12 baadaye, juzi Jumamosi jioni, Gerrard alikuwa akicheza dhidi ya Arsenal na alipika mabao mawili ya kwanza. Hakuwa na cha kujivuna wala kujifunza kutoka kwa kiungo yeyote wa Arsenal.


Kwanini? Kama angekuwa anajifunza kutoka kwa kiungo yeyote wa Arsenal, basi asingeweza kuwa mmoja kati ya viungo mahiri duniani kama alivyofuata nyayo za Patrick Vieira enzi zake.


Arsenal soft, Arsenal soft


Arsenal walikuwa walaini, hasa sehemu ya kiungo. Kocha wao, Arsene Wenger, anategemea zaidi ubora wa wachezaji wake kuliko uimara wa wachezaji wake.


Kwa kusoma majina kwenye karatasi, ni mchezaji mmoja tu wa Liverpool anaweza kucheza kikosi cha Arsenal kwa sasa, Luis Suarez.


Lakini kwa kuangalia uimara wa timu na nguvu ya kujituma, ni wachezaji wawili tu wa Arsenal wangeweza kucheza katika kikosi cha Liverpool katika mechi hiyo, ni Jack Wilshere na Alex Oxlade-Chamberlain.


Wenger ameiua Arsenal ya wachezaji wagumu kama vile Vieira, Manu Petit, Fredrick Ljungberg, Ray Parlour, Tony Adams na wengineo. Hawa walikuwa na ubora kama wachezaji na imara kama watu wa Manchester City ya sasa. Sasa anawategemea zaidi wachezaji wenye ubora. Lakini ameshindwa kuwatia uimara wa kuhimili mikiki ya mechi kubwa, au zile ndogo ambazo zinachezwa na timu zenye roho ya paka.


Arsenal inataka kucheza mechi kwa jinsi inavyojisikia yenyewe na si jinsi mpinzani anavyocheza. Haiwezi kupaki basi na kuvuta subira ya mechi wakati wakianza kujipanga taratibu.


Katika mechi kubwa, unahitaji wachezaji wenye roho ngumu zaidi kuliko wenye ubora. Wenger hataki kutengeneza wachezaji wa aina hii na ndio maana ametengeneza kikosi cha mechi ndogo na si cha mechi kubwa. Hauwezi kuwa bingwa kwa kufungwa 6-3 na Manchester City kisha ukafungwa 5-1 Anfield halafu utazamie kuchukua ubingwa. Sijawahi kuona timu ikipata matokeo ya aina hii ndani ya msimu mmoja na kisha ikatazwa kuwa bingwa

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright WORLD OF TODAY Published.. Blogger Templates
Back To Top