WENGER Akiri Ligi Kuu England imefika pagumu







Ligi Kuu England (EPL) imefika katika mzunguko wa 25 na kwa kweli ni pagumu.


Ni vigumu kutabiri timu gani itachukua ubingwa pia zipi zitashuka daraja. Hii ni kutokana na matokeo yanavyochanganya.


Manchester City iliyosifika kwa upachikaji wa mabao mengi kuliko timu nyingine, imekumbwa na hofu kutokana na matokeo ya mechi zake mbili zilizopita.


Kufungwa na Chelsea nyumbani ikiwa ndio mechi ya kwanza waliyopoteza Etihad tangu kuanza msimu huu na kwenda suluhu na timu dhaifu ya Norwich City, kunaacha maswali mengi.


Vijana hao wa Manuel Pellegrini, wapo nafasi ya tatu katika msimamo wa ligi hiyo huku wakiwa bado na mechi ngumu ugenini na inatabiriwa kwamba wanaweza kudhoofishwa zaidi.


Kocha Jose Mourinho ‘The Happy One’ wa Chelsea kudai kwamba timu yake haipo kwenye mbio za ubingwa, inaonekana kama utani.


The Blues wameimarika sana na mfululizo wao wa ushindi umewaweka pazuri, wakiongoza ligi sasa halafu wakiwa wanajiamini zaidi.


Arsenal iliyokuwa inaongoza ligi kwa muda mrefu na tena kwa tofauti kubwa ya pointi, imeanza kunyong’onyea. Ilitoka sare na timu isiyotarajiwa na kisha kuja kubugizwa mabao 5-1 na Liverpool.


The Gunners na Manchester City zinaweza kujitetea kwamba hali yao inasababishwa na wachezaji wao muhimu kuwa majeruhi, lakini walikuwa na nafasi na walisajili wachezaji wengi.


Kwa Sergio Agueri kukosekana Manchester City na Theo Walcott kuwa majeruhi Arsenal, hakumaanishi kwamba hakuna wengine.


Lakini inavyoelekea ni kwamba athari za kukosekana kwao ni kubwa ijapokuwa bado wana nafasi nzuri ya kuliendea taji la ligi hii maarufu zaidi duniani. Timu hizo zinapishana kwa pointi moja moja tu, Chelsea wakiwa juu wakifuatiwa na Arsenal na Manchester City huku Liverpool ikija kwa mbali kidogoread more...........

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright WORLD OF TODAY Published.. Blogger Templates
Back To Top