JAJI AUGUSTINE RAMADHAN ATAJA MIPAKA YA BUNGE LA KATIBA,Soma hufaamu mipaka ya bunge la katiba

 
Jaji Agustino Ramadhani. PICHA|MAKTABA 




 Jaji Mkuu mstaafu, Augustine Ramadhani, amesema Bunge Maalumu la Katiba linabanwa na Sheria ya Mabadiliko ya Katiba Kifungu cha 25 kufanya mabadiliko makubwa ya Rasimu ya Pili ya Katiba iliyofwasilishwa bungeni.

Akifungua mkutano mkuu wa Chama cha Wanasheria wa Tanganyika(TLS) jana jijini hapa, Jaji Ramadhani, alisema hata hivyo kutokana na malumbano ya kisheria yaliyoibuka sasa ni vyema wabunge wa Bunge hilo wakaachiwa jukumu wenyewe kukipitia kifungu hicho cha 25, ili kuona mamlaka yao.


“Kuna wasomi wengine kama Profesa Issa Shivji, wanasema Bunge lina madaraka ya kufanya mabadiliko, lakini madaraka ya Bunge yanapatikana Kifungu cha 25 cha Mabadiliko ya Katiba. Tuliachie Bunge lenyewe kusoma kifungu na kuona madaraka yao bila sisi kusema. Huu ni msimamo wangu mimi,”alisema Jaji Ramadhani.


Hata hivyo, aliwataka wabunge wa Bunge hilo, kufikia uamuzi sahihi wa kupatikana Katiba Mpya bila kutanguliza mbele misimamo ya vyama vyao.


Jaji Ramadhani alisema ni lazima sasa kuwepo na mabadiliko, kwani kila kitu kinaenda na wakati akakumbushia kauli ya Rais mstaafu Alli Hassan Mwinyi kuwa kila enzi ina kitabu chake.


“Tumekaa miaka 50 na kitabu hiki lazima sasa tubadilike kuangalia miaka 50 mingine twende na kitabu gani, ila tubadilike kwa masilahi ya umma siyo kusimamia misimamo ya kivyama tu” alisema.


Jaji Ramadhani aliongeza kuwa wajumbe wa Bunge la Katiba wanapaswa kuangalia, mustakabali wa taifa katika uamuzi wao.


Atetea mfumo wa Serikali tatu


Akizungumzia muundo wa Muungano ambao umekuwa na malumbano makubwa, Jaji Ramadhani alisema tume yao ilifanya kazi kwa uadilifu mkubwa na kufikia uamuzi wa kuwa na muundo wa Serikali tatu.


Alieleza upungufu mbalimbali katika mfumo wa sasa ukiwapo wa kisheria na kufafanua mapendekezo wa Serikali tatu yalitokana na maoni ya wananchi wa Tanzania Bara na Visiwani waliopendekeza muundo wa aina tano ya Muungano.


“Wapo waliotaka Serikali moja, wengine Serikali mbili, wengine Serikali tatu, wapo waliotaka Serikali nne ikiwepo Serikali ya Pemba na wapo waliotaka muundo wa Muungano wa mkataba sasa wote walisikilizwa,” alisema.


Jaji Ramadhani, alisema tume yao, ambayo ilikuwa na watu wa kada mbali mbali na ujuzi wa aina tofauti, akiwepo yeye ambaye amewahi kuwa Jaji Mkuu wa Zanzibar na Tanzania, wanaamini uamuzi wa muundo wa Serikali tatu unaweza ukawa ndiyo mwafaka kwa sasa. Soma zaidi

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright WORLD OF TODAY Published.. Blogger Templates
Back To Top