MUGABE ATIMIZA UMRI WA MIAKA 90. HUU HAPA HUSIA WAKE KWA VIONGOZI WA AFRIKA

 
Mugabe 


Harare. Rais mkongwe wa Zimbabwe, Robert Mugabe ambaye ameiongoza nchi hiyo tangu mwaka 1980, ametimiza miaka 90.


Rais huyo ambaye ndiye pekee aliyekaa madarakani kwa muda mrefu Afrika mpaka sasa leo anatarajiwa kufanya sherehe kubwa ya kutimiza umri wake huo, ambao ulitimia rasmi jana, Februari 21.


Chama tawala cha nchi hiyo ZANU-PF kimeandaa sherehe ya kipekee ya kuzaliwa Rais huyo ambayo itafanyika kwenye Uwanja wa soka wa Marondera.


Watumishi wa Serikali walikuwa wakikatwa kiasi cha dola mbili kwa ajili ya maandalizi ya sherehe hiyo inayotarajiwa kugharimu kiasi cha dola milioni moja.


Mugabe aliingia madarakani mwaka 1980 baada ya nchi hiyo kupata uhuru wake kutoka utawala wa kikoloni wa Uingereza wakati huo ikiitwa Southern Rhodesia mpaka kuwa Zimbabwe kama taifa huru.


Rais Mugabe anasherehekea umri huo huku dunia na Afrika kwa jumla wakiitazama sherehe hiyo kwa mitazamo tofauti, kutokana na umri alionao tangu alipoiwezesha Zimbabwe kupata uhuru akiwa kiongozi wa taifa hilo mpaka leo hii.


Vyombo vya habari vya kimataifa vinammulika Rais Mugabe kama mtu asiyeyumbishwa kutokana na misimamo yake dhidi ya mataifa ya Magharibi.


Mugabe ambaye alizaliwa Februari 21, 1924, ana mengi ya kujivunia katika utawala wake ambao umekuwa ukipitia milima na mabonde likiwamo suala la kuporomoka uchumi wa nchi hiyo kutokana na kuwekewa vikwazo na nchi za Ulaya.


Rais huyo anapoadhimisha sherehe ya kuzaliwa kwake leo, atakumbukwa kwa kauli zake zenye utata dhidi ya viongozi wa mataifa ya Magharibi na msimamo wake kuhusu mashamba makubwa nchini humo.


Msimamo wake huo ulisababisha kutolewa maazimio ya Umoja wa Ulaya kuhusu kufungiwa kutokanyaga katika ardhi ya Ulaya.


Wiki hii wakati Rais Mugabe akijiandaa kusherehekea siku yake hii ya kuzaliwa alikwenda Singapore kwa ajili ya matibabu ya macho ili kuondolewa mtoto wa jicho, tatizo linalomsumbua kwa muda mrefu sasa.


Taarifa rasmi ya Ikulu ya nchi hiyo kupitia kwa msemaji wa Mugabe, George Charamba ilisema rais huyo anakwenda kufanyiwa upasuaji wa pili lakini safari hii ni kwa ajili ya kusafisha jicho lake la kushoto. Soma zaidi

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright WORLD OF TODAY Published.. Blogger Templates
Back To Top