Sekta ya mawasiliano nchini inakua kwa kasi baada ya milango kufunguliwa mwaka 2005 na kusababisha kuongezeka kwa idadi ya watoa huduma za mawasiliano pamoja na watumiaji.
Kutokana na kuongezeka kwa idadi ya watoa huduma za simu, Serikali inaendela kupata mapato na kukuza sekta nyingine za kiuchumi kutokana na huduma za mawasiliano kuwa rahisi.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Profesa John Nkoma anazungumzia kwa kina jinsi mamlaka hiyo ilivyotumia fursa ya ukuaji huo na kuisaidia Serikali kuongezea mapato zaidi tofauti na ilivyokuwa ikifikiriwa awali.
“TCRA imefanikiwa kuilipa hazina Sh1.6 bilioni ikiwa ni mgawo wa Oktoba, mwaka jana kwa mujibu wa sheria ya TTMS, pia tumekabidhi malipo ya Sh1.6 bilioni zikiwa ni mgao wa Novemba,” anasema Nkoma.
Profesa Nkoma anasema hayo mbele ya Rais Jakaya Kikwete wakati wa hafla ya uzinduzi Mtambo Maalumu wa Kusimamia na Uhakiki wa Mawasiliano ya Simu, (TTMS), iliyofanyika hivi karibuni kwenye Ofisi za Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Dar es Salaam.
Anafafanua kuwa mapato hayo hayakuwapo kabla ya kufungwa kwa mtambo huo, hivyo kwa kiasi kikubwa Serikali imeongeza mapato yake.
“Jambo hili ni jema na linatufanya tutembee kifua mbele, kwani Serikali yetu sasa inapata mapato yake kama ambavyo ilikuwa inastahili,” anasema Profesa.
Kwa upande wake, Rais Kikwete anaeleza kufurahishwa na hatua hiyo, na anatumia nafasi hiyo kuwapongeza TCRA kwa hatua hiyo akieleza kuwa inawezesha uchumi wa nchi kupata kichocheo cha kukua, kwa kuwa sasa kutakuwa na udhibiti wa mawasiliano hasa ya simu za nje ya nchi na kuongeza kipato kwa taifa.
Rais Kikwete pia anaiagiza Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo kuhakikisha mchakato wa sheria ya usalama kwenye mitandao unakamilika na kuanza kutumika ili kudhibiti wanaotoa siri za nchi kwa kisingizio cha uhuru wa habari.
Serikali ilivyokosa mapato
Anasema awali watoaji wa huduma za mawasiliano ya simu za kimataifa ndiyo walikuwa wakipanga bei kwa makubaliano na kampuni za nje na simu zinazopigwa kuingia nchini (bilateral arrangements).
Kampuni hizo za mawasiliano zenye leseni za kutoa huduma za simu za kimataifa ni Airtel, Mic (tiGo) Sixtelecoms, Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Vodacom na Zantel. endelea.............
Post a Comment