
Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kuchukua fomu, Sitta alisema viwango na kasi ni sehemu ya maisha yake.PICHA|MAKTABA
Dodoma. Wakati Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta akichukua kwa mbwembwe fomu za kuwania nafasi ya uenyekiti wa Bunge Maalumu la Katiba jana, wajumbe
wengine watatu nao wamejitokeza kuwania nafasi hiyo.
Katibu wa Bunge, Dk Thomas Kashillilah, alilieleza gazeti hili kuwa, wajumbe waliojitokeza jana
hiyohiyo kuchukua fomu ni, Hashim Rungwe wa NCCR-Mageuzi, Dk Terezya Huvisa wa CCM na Mwenyekiti wa Chama cha Tadea, John Chipaka.
Wajumbe hao walichukua fomu hizo katika ofisi ya Katiba ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania jana mchana, huku mchakato wa wake ukielezwa kuendelea hadi saa 4 asubuhi ya leo.
Sitta na Hashim Rungwe, walipatikana jana kuzungumzia hatua yao hiyo, lakini Chipaka na Dk. Huvisa hawakupatikana. Hata walipotafutwa kwa njia ya simu zao za mkononi,simu ziliita bila ya kujibiwa.
Mbwembwe za Sitta
Wakati wajumbe hao wakichukua fomu, Sitta alisambaza vipeperushi vya kuomba kura vikiwa na rangi za njano na bluu.
Katika kila ukurasa wa vipeperushi hivyo, ilielezwa kuwa atafanya kazi zote kwa viwango na kasi.
Katika vipeperushi hivyo, Sitta mwenye shahada ya sheria, anasema aliwahi kuwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano, aliyesimamia mabadiliko makubwa ya kanuni yaliyoimarisha uhuru na demokrasia ya Bunge.
Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kuchukua fomu, alisema viwango na kasi ni sehemu ya maisha yake.
“Hata Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki, nasimamia kwa kuzingatia viwango na kasi. Hata Bunge hili ukitaka utendaji bora lazima ufikie viwango vyake, ili yale unayoyafikiria yawafikie watu ndani ya wakati, siyo viwango bora huku shughuli hazimaliziki,”alisema Endelea...........
Post a Comment