MWENYEKITI wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba, amesema baadhi ya taasisi za kiserikali, ama moja kwa moja au kwa tafsiri ya mapendekezo yao, zilipendekeza au kukubali muundo wa serikali tatu.
Akiwasilishaji rasimu ya Katiba Mpya katika Bunge Maalumu la Katiba jana Jumanne, mjini Dodoma, Warioba alizitaja taasisi hizo kuwa ni Baraza la Wawakilishi Zanzibar lililopendekeza kuwapo kwa mamlaka huru ya Zanzibar, mamlaka huru ya Tanganyika na mamlaka ya Muungano na kutaka maeneo, uwezo, nguvu, utendaji na mipaka ya kila mamlaka iwekwe wazi.
“Baraza la Wawakilishi na Ofisi ya Makamu wa Rais zilipendekeza kuhusu Muundo wa Serikali kwamba, nanukuu... kuwe na Rais mmoja wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Wakuu wa Serikali za Washirika wa Muungano wapewe vyeo vingine vinavyoendana na hadhi na mamlaka zao. Pia katika kutaja hizo serikali tatu inabidi zitenganishwe ili Serikali ya Muungano ionekane ndio ya juu,” alifichua siri hiyo Jaji Warioba ambayo hakuwahi kuiweka hadharani kabla.
Alisema hata ofisi ya Waziri Mkuu kupitia Baraza lao ilipendekeza, kuhusu uongozi wa taifa kwamba kuwe, na “Rais wa Jamhuri ya Muungano, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano, Waziri Mkuu wa Serikali ya Tanganyika na Waziri Mkuu wa Serikali ya Zanzibar. Mapendekezo hayo ni kwa sababu hakuna umuhimu wa kuwa na marais watatu (3) katika nchi moja na wala neno Rais halimuongezei hadhi kiongozi yeyote.
“Pia kutoa nafasi kwa mawaziri wakuu kuwa watendaji zaidi na hivyo kusimamia serikali za washirika.”
Alisema hata Bunge la Jamhuri ya Muungano katika maoni yake lilipendekeza kuwa na Tume ya Utumishi wa Bunge ambayo inajumuisha, katika wajumbe, Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano (Mwenyekiti), Spika wa Bunge la Tanzania Bara na Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar.
Kutokana na hayo, Warioba alisema; “Baada ya kuona takwimu hizi na kuchanganua sababu zilizotolewa na makundi mbalimbali, Tume iliamua kufanya utafiti wa kina kuhusu muundo wa Muungano na matatizo yake tangu Muungano ulipoundwa.
Matokeo ya utafiti
Kutokana na utafiti huo, Warioba alisema mambo kadhaa yalijitokeza. Mambo hayo ni kama ifuatavyo:
Kwanza, kulikuwa na changamoto nyingi baada ya Tanganyika na Zanzibar kuungana mwaka 1964. Ujenzi wa taasisi ili kuendesha mambo ya Muungano ulikuwa ni changamoto kubwa.
Alisema Serikali ya Muungano haikuwa na taasisi zake kwa hiyo ilianza kwa kutumia taasisi zilizokuwapo katika sehemu zote mbili za Muungano.
“Kwa upande wa sheria, hali ilikuwa hivyo hivyo. Hata uamuzi wa kuifanya Tanzania kuwa nchi ya demokrasia ya chama kimoja ulichukuliwa wakati nchi ikiwa na vyama viwili; TANU na ASP. Kwa hiyo, kila upande uliendesha mambo yake kutumia itikadi na sera zake,” alisema.
Alisema changamoto hizo hazikuzuia kuimarika kwa Muungano kwa sababu utashi wa kisiasa wa waasisi wa Muungano ulikuwa mkubwa.
“Mwaka 1977, vyama vya siasa vya TANU na ASP viliunganishwa na Chama cha Mapinduzi kilizaliwa na Katiba ya kudumu ilitungwa. Baada ya Jumuiya ya Afrika Mashariki kuvunjika, baadhi ya mambo yaliyokuwa chini ya Jumuiya hiyo yaliwekwa kwenye Orodha ya Mambo ya Muungano,” alisema akiongeza kwamba matokeo ya hatua hizo, nchi ilionekana ni moja, yenye mshikamano, utulivu na amani.
“Wakati huo, viongozi na watumishi wa umma na kwenye chama cha siasa walipangiwa kazi sehemu yoyote ya nchi bila kujali sehemu wanayotoka.
Kwa muda mfupi nchi ilionekana kuwa kweli ni taifa moja. Lakini hali hiyo haikudumu kwa muda mrefu. Utaifa wa nchi mbili ukaanza kujitokeza. Viongozi na watumishi wa umma kutoka upande mmoja wa Muungano wakaonekana hawapendi kwenda kufanya kazi upande wa pili wa Muungano.
“Pia majina ya sehemu mbili za Muungano yakabadilishwa. Badala ya Tanzania Bara na Tanzania Visiwani tukaanza kutumia Tanzania Bara na Tanzania Zanzibar, ili kulinda Zanzibar isionekane imemezwa. Ni wakati huo, lugha ya Tanganyika kuvaa koti la Muungano ilianza kusikika,” alisema.
Aliongeza: Mwaka 1984, kulitokea kile kilichoitwa “kuchafuka kwa hali ya hewa ya kisiasa Zanzibar” msingi wake ilikuwa ni mpango wa baadhi ya viongozi wa Zanzibar kutaka serikali tatu, ingawa jaribio hili halikufanikiwa, Zanzibar ilitunga Katiba mpya mwaka huo huo.
Alisema katika Katiba hiyo, Zanzibar iliondoa madaraka ya sheria zinazotungwa na Bunge kutumika moja kwa moja Zanzibar.
“Katiba ya Zanzibar iliweka masharti kwamba sheria za Muungano zipelekwe kwenye Baraza la Wawakilishi kabla ya kutumika Zanzibar

“Katiba ya Zanzibar iliweka masharti kwamba sheria za Muungano zipelekwe kwenye Baraza la Wawakilishi kabla ya kutumika Zanzibar - See more at: http://raiamwema.co.tz
Post a Comment