Urais 2015 waitikisa nchi, sitta nae asema yake,




Akizungumza kwenye Mahafali ya Chuo cha Uuguzi cha Masista wa Kanisa Katoliki Kanosa Mugana, Wilaya ya Misenyi, Mkoa wa Kagera jana, Sitta alisema wengi wa waliotangaza nia hawafai na kwamba wanapiga porojo tu.PICHA|MAKTABA 
Dar es Salaam/Misenyi. Mjadala wa urais mwaka 2015 unaonekana kuanza kuitikisa nchi kutokana na vigogo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuendelea kujitokeza hadharani na kutangaza nia, huku wasomi, viongozi wa dini, wanaharakati na vyama vya siasa wakitaja sifa za mgombea.


Mmoja wa vigogo hao wa CCM ni Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta ambaye jana alijitokeza na kusema atajitosa kwenye kinyang’anyiro cha urais iwapo wataendelea kujitokeza wasiokuwa na sifa.


Akizungumza kwenye Mahafali ya Chuo cha Uuguzi cha Masista wa Kanisa Katoliki Kanosa Mugana, Wilaya ya Misenyi, Mkoa wa Kagera jana, Sitta alisema wengi wa waliotangaza nia hawafai na kwamba wanapiga porojo tu.


Sitta alisema wengine wamejitokeza kwa ‘gia’ ya ajira, lakini hawabainishi chanzo chake, kwani tatizo hilo limetokana na ufisadi kwa baadhi ya viongozi.


Aliwataka wananchi kuwapima wagombea kwa makini kwani wapo baadhi yao wanajinadi kuwa wao ni vijana kitu ambacho siyo kigezo cha kuwa rais.


“Ndugu zangu Watanzania, tusipowachuja watu kwa chujio la tabia zao, tutaangukia mtego wa kuwapima watu kama vile tunafanya mzaha, maana kuna wengine wameanza kusema nichagueni mimi ni kijana, hivi kwani urais ni mashindano ya ulimbwende, tunatafuta mzuri?” alihoji.


Awaponda waliotangaza nia


Alisema akiangalia orodha ya waliojitokeza haifai na kwamba, labda watu kama wawili wanaoweza kuungwa mkono lakini hakuwataja.


Waziri Sitta alitumia hadhara hiyo kuihadharisha jamii kuona suala la uchaguzi wa rais kama jambo la kawaida, kwani ikicheza nchi itazama.


”Niseme jingine, kwa kuwa nikitazama hiyo anga ya hawa wanaotafuta ukubwa, nawaona kama mmoja wawili ndiyo kidogo unaweza kuwaunga mkono. Hali hii ikiendelea namna hii, eeh itabidi na sisi wazee tujitose manake ikiwa watu wenyewe hawa ni walaghai, wengine ni waongo, wengine rekodi mbaya, wengine walishiriki kuhujumu nchi, ndiyo wanakwenda kimbelembele wanapigana vikumbo.


Wasomi, wanaharakati Wakati Sitta akisema hayo, wasomi, wanasiasa na wanaharakati wamesema rais ajaye anatakiwa kuwa mzalendo, msomi, mwadilifu, mchapakazi, anayejua matatizo ya nchi na wananchi na akubali kuyatatua, asiwe mbaguzi, mwenye uamuzi mgumu, anayetanguliza masilahi ya taifa mbele na atakayepambana na rushwa na ufisadi kwa vitendo

soma zaidi, bofya hapa 

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright WORLD OF TODAY Published.. Blogger Templates
Back To Top