Mtei: Nililipwa mshahara sawa na Mwalimu Nyerere,


Mtei ambaye pia aliwahi kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha kabla ya kuteuliwa kuwa Gavana wa BoT alisema katika mazingira ya sasa hakuna kiongozi yeyote ambaye anaweza kukubali au kupunguza mshahara wake.PICHA|MAKTABA

Arusha. Inawezekana likawa jambo nadra kutokea kwa sasa, lakini enzi za uongozi wa Mwalimu Julius Nyerere lilitokea.


Ni baada ya mwasisi huyo wa Taifa kuamua kwa hiari kupunguza mshahara wake kwa asilimia 10 ili kupunguza pengo baina ya maskini na wale wenye kipato cha juu, uamuzi ambao ulifuatwa na aliyekuwa Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) wakati huo, Edwin Mtei.


Mwaka 1968, Mwalimu Nyerere aliyekuwa akilipwa mshahara wa Sh5,000 kwa mwezi alikiona ni kiasi kikubwa ikilinganishwa na wengi wa watumishi na hivyo kuamua kukipunguza.


Mshahara huo wa Mwalimu Nyerere ni sawa na ambao alikuwa akilipwa pia Gavana Mtei. Kutokana na punguzo hilo, mishahara yao ilishuka hadi Sh4,500 kwa mwezi.


Akizungumza katika mahojiano maalumu na gazeti hili nyumbani kwake Tengeru, nje kidogo ya Mji wa Arusha Jumatatu iliyopita, Mtei alisema alifikia uamuzi huo wa kupunguza mshahara wake baada ya Mwalimu Nyerere kutangaza kupunguza mshahara wake.


Alisema: “Nilipunguza mshahara wangu tena kwa hiari yangu baada ya kuona Mwalimu Nyerere amepunguza wa kwake.”


Alisema wakati ule mshahara wa Gavana ulikuwa ukipangwa na Serikali na kwamba ulikuwa na kipengele katika mkataba kikionyesha kuwa hauwezi kupunguzwa na mamlaka yoyote, labda atakapotaka mwenyewe.


Mtei ambaye pia ni mwasisi wa Chadema alisema sababu nyingine iliyomsukuma kupunguza mshahara wake ni kuona kwamba kama asingefanya hivyo, basi angemzidi mshahara Rais (Nyerere), kitu ambacho kwake hakukipenda.


Alisema, ingawa Mwalimu Nyerere alipunguza mshahara, lakini yeye kisheria hakuwa akibanwa kufanya hivyo kutokana na mkataba wake ambao ulikuwa ukiibana Serikali kutokuugusa mshahara wake.


Alieleza kuwa ukimwondoa yeye na Mwalimu Nyerere, Serikali iliamua kuwapunguzia mishahara watumishi wengine wa kada nyingine serikalini ili kubana matumizi.


“Watu wote walipunguziwa mishahara kuanzia vigogo wote (wa wakati ule),” alisema Mtei ambaye Jumamosi iliyopita alitimiza miaka 82 tangu kuzaliwa kwake.


Sababu za punguzo hilo

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright WORLD OF TODAY Published.. Blogger Templates
Back To Top